Habari za Punde

Nani atawika fainali Kiev kati ya Salah, Ronaldo na Milner

Fainali ya Champions League itakuwa kati ya timu ambazo zimefunga mabao mengi zaidi msimu huu huku washambuliaji bora zaidi duniani wakikutana.
Real Madrid wanatafuta ushindi wa 13 na wa tatu mfulizo huku Liverpool wakiweza kupanda juu ya Bayern Munich na Barcelona nyuma na AC Milan katika orodha ya vilabu vilivyopata ushindi mara nyingi zaidi katika European Cup na Champions League ikiwa wataibuka washindi huko Kiev.
Milner anaweza kuwa na umuhimu usiotarajiwa Kiev?
Zikiwa zimefunga zaidi ya mabao 90 kwenye mashindano yote msimu huu ni wazi kuwa fainali hii itakuwa kama vita kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Mohamed Salah wa Liverpool.
Wote wako mbioni kun'gang'ania tuzo la Ballon d'Or mwishoni mwaka 2018, lakini pia kuna mwanamume ambaye bila kutarajiwa huenda akawa mwenye umuhimu mkubwa huko Kiev.
James Milner alionyesha ubabe wakati wa nusu fainali dhidi ya Roma wakati alifikisha mchango wake muhimu katika mechi hadi mara 8 msimu huu na kusawazisha rekodi iliyowekwa na Neymar mwaka 2016-17.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.