Habari za Punde

Uzinduzi wa Bonaza la Kuchangia Damu Kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Lafani na Kupiga Idadi Iliokusudiwa.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akihutubia wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Bonaza la Kuchangia Damu kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi lililofanyika katika Viwanja vya Baraza Chukwani Zanzibar kushoto Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na kulia Katibu wa Baraza Mhe. Raya Issa Msellem.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Bonaza la kuchangia Damu kwa Wajumbe wa Baraza na Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo lililofanyika katika viwanbja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Bonaza la kuchangia Damu kwa Wajumbe wa Baraza lililofanyika katika Viwanja vya Baraza Chukwani Zanzibar.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Raya Issa Msellem akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa kuchangia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akizindua Bonaza la Kuchangia Damu kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar lililofanyika katika viwanja vya Baraza Chukwani Zanzibar na kupita lengo lililowekwa la kuchangia Damu kwa Wajumbe na Wananchi walioshiriki zoezi hilo lililoendesha na Kituo cha Damu Salama Zanzibar.

Mwandishi wa TBC Zanzibar Awadh akishiriki katika kuchangia Damu wakati wa Bonaza la Kuchangia Damu kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar lililofanyika katika viwanja vya Baraza Chukwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.