WAZAZI na Walezi mkoani Tanga wametakiwa kuhakikisha wanawapa watoto wao
zawadi kwenye kpindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuwaingiza
kwenye mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na matibabu wakati
wanapougua.
Hayo yalisemwa na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
(NHIF) Macrina Clemens (Pichani Juu) ambapo alisema zawadi hiyo ni
muhimu sana katika ukuaji wao badala ya kuwanunulia nguo ambazo wanavaa
kwa wakati Fulani na baaadae kwisha.
Alisema mpango huo ni muhimu kwa watoto wao kutokana na kuwahakikishia
kupata huduma za matibabu wakati wote wanapokumbana na magonjwa
mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri.
“Ndugu zangu wazazi na walezi kwenye kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani
zawadi mzuri ambayo mnaweza kuwapatia watoto wenu ni kuwaingiza kwenye
mpango huu wa Toto Afya Kadi kwani malipo yake yana muwezesha mtoto
kupata huduma za matibabu mwaka mzima kwa kiasi cha sh.50400”Alisema.
Hata hivyo alisema wataendelea kuhimiza wananchi kuweza kuwaingiza
watoto wao kwenye mpango huo ili waweze kuwahakikishia watoto wao kupata
huduma za matibabu bila vikwazo hasa wanapokuwa wakiumwa .(Habari kwa
Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment