Habari za Punde

BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019 YAPITA KWA KISHINDO BUNGENI JIJINI DODOMA

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia-mbele), wakati wa Kikao cha Bunge kilichopitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 32.48 kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ndani ya ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma, kabla ya Bunge kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikai ya shilingi trilioni 32.48 kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Baadhi ya wabunge wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 Bungeni, Dodoma ambayo imeweka kipaumbele katika maendeleo ya  uchumi wa viwanda.  
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto), akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati), baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 Bungeni Dodoma.
Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, (kulia) akibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi wa Bajeti wa Wizara hiyo Bw. Pius Mponzi (katikati), nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wakiwa na furaha katika viwanja vya Bunge baada ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 kupita Bungeni Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa pili kushoto), pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Bunge kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono wa pongeze na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.