Habari za Punde

Kombe la Dunia 2018: Didier Drogba Azungumzia Manufaa ya Kunyoa Nywele, na Nchi za Afrika Zinavyocheza Urusi

Mchezaji wa zamani wa Ivory Coast na Chelsea Didier Drogba amesema watu hawafai kushangazwa sana na hatua yake kunyoa nywele ingawa amekiri maisha yake yameimarika.
Aidha amezungumzia uchezaji wa klabu za Afrika katika Kombe la Dunia.
Kuhusu hatua yake kukata nywele zake, amesema hilo halikuwa jambo la ajabu sana kwake.
"Ni jambo nililokuwa nimelifanya miezi kama saba hivi iliyopita, lakini nafikiri mimi si mzuri sana katika kuweka mambo mitandao ya kijamii - huwe siwezi selfie za kutosha," amesema.
"Kwa hivyo, ninajua ni jambo watu wengi hawajalizoea, kwa sababu nilikuwa na nywele ndefu kwa miaka mingi - lakini kuwa bila nywele ndefu si jambo geni."
Amesema hata hivyo kwamba "huwa inarahisisha mambo."
"Kwa sababu sasa huwa situmii muda mwingi kwenye bafu," amesema Drogba akihojiwa na BBC.

'Afrika hawachezi kama timu'

Mataifa ya Afrika hayajapata matokeo ya kuridhisha Kombe la Dunia isipokuwa Senegal na Nigeria ambao wameshinda mechi moja kila mmoja.
Misri na Morocco tayari zimeyaaga mashindano na matumaini ni finyu kwa Tunisia baada yao kushindwa 5-2 na Ubelgiji mechi yao ya pili.
Drogba anasema Nigeria, mechi yao dhidi ya Iceland, walicheza jinsia anavyotaka kuona nchi za Afrika zikicheza "kwa kushambulia, kutumia kasi na nguvu, na kushambulia goli mara nyingi."
Anasema hilo halikuwepo walipochapwa na Croatia mechi yao ya kwanza.
"Walikuwa wanacheza wenyewe - kujiweka sawa, kujilinda bila kushambulia, na kwa kutoa pasi sehemu moja ya uwanja hadi nyingine," amesema.
"Wakati huu (dhidi ya Iceland) walicheza kushinda. Walikuwa na washambuliaji wawili na walikuwa na kasi sana na ukali wakishambulia kiasi kwamba Iceland waliingiwa na asiwasi.
Walikuwa hawatabiriki kwa mashambulizi na walivutia sana.
"Nilitarajia wacheze hivi Kombe la Dunia - na ndio maana wakashinda mechi hiyo," anasema.
Anaongeza kuwa mataifa ya Afrika yakicheza Kombe la Dunia yanafaa kudumisha utambulisho wao kama time, na anasema ni Senegal pekee waliokuwa wamefanikiwa kufanya hivyo kabla ya Nigeria mechi yao ya pili.
"Ni muhimu kwao kuendelea kufanya hivyo - na Nigeria pia - ili wafike hatua ya 16 bora. Wakiamua kucheza mchezo wa kujilinda na kuanza kuogopa kufungwa, watarudi nyumbani."
DrogbaHaki miliki ya pichaTWITTER @DIDIERDROGBA
'Namuelewa Mo Salah, yalinitokea 2010 Afrika Kusini'
Drogba amesema pia anafahamu mambo yalivyokuwa kwa Mohamed Salah kutokuwa sawa wakati wa Kombe Dunia.
"Namfahamu vyema kutoka kwa wakati wetu Chelsea, ambapo alikuwa kama kaka mdogo kwangu, na najua anachoongeza kwenye timu ya Misri," anasema.
Anaeleza kwamba Misri pia hujihisi wako salama akiwa uwanjani.
"Nimeyapitia kama hayo nilipovunjika mkono kabla ya Kombe la Dunia 2010. Kama salah, nilicheza - lakini sikuwa karibu asilimia 100 kuwa sawa wakati Kombe la Dunia unahitaji kuwa sawa asilimia 120".
Ingawa Morocco wanarudi nyumbani, anasema walijaribu mechi yao dhidi ya Ureno.
Amekubaliana hata hivyo na kocha wa England Gareth Southgate kwamba la Tunisia ni ngumu mno. Anasema tangu mwanzo alitarajia Ubelgiji na England wasonge hadi hatua ya muondoano.'England, Croatia na Ubelgiji'
Drogba anasema ingawa anawapenda England, na alifurahishwa na uchezaji wao dhidi ya Tunisia, ni mapema sana kwao kupigiwa upatu.
Anasema amependezwa piana Croatia, na viungo wao wa kati - Ivan Rakitic, Luka Modric na Ivan Perisic - waliocheza vyema sana dhidi ya Argentina.
Lakini anapendezwa zaidi na Ubelgiji kufikia sasa. Sababu ya kwanza ni kwamba ana marafiki wengi kikosi hicho, lakini anasema wana ustadi mwingi na uzoefu na wanacheza vizuri sana.
"Sijui ni kwa nini watu wengi hawawaangazii kama wanaotarajiwa kushinda," anasema.'Mshambuliaji ni kujituma'
Drogba anasema ingawa tumeshuhudia mataifa mengi yanayodhaniwa kutokuwa stadi kwa mpira yakiwaangusha miamba, kilichompendeza zaidi ni uchezaji wa kushambulia.
Anasema amefurahishwa zaidi na uchezaji wa Cristiano Ronaldo wa Ureno aicheza dhidi ya Uhispania ambapo alifunga mabao matatu, na Ahmed Musa wa Nigeria aliyefunga mawili dhidi ya Iceland.
"Wote wawili walikuwa na nia ya kujaribu, na hawakuwa na wasiwasi wa kukosa," anasema.
Anaeleza pia kwamba amefurahishwa na teknolojia inayowasaidia waamuzi, maarufu kama VAR ambayo imechangia uamuzi wa kutoa penalti mara kadha.
"Mnaweza mkafikiria nazungumza kama mshambuliaji wa zamani hapa - lakini kusema kweli imewafaa mabeki pia. Inapunguza makosa pande zote mbili."
Anaamini alifikiri mara ya kwanza kwamba Neymar alifaa kupewa penalti dhidi ya Costa Rica, lakini uamuzi uliotolewa ulikuwa sahihi kwa sababu hakukuwa na nguvu za kutosha kumwangusha.
"Ni maamuzi kama haya ambayo yanaathiri mechi ambayo ni muhimu sana kuwa sahihi."
"Kuwa na VAR katika Kombe la Dunia la sasa umekuwa ni uvumbuzi na uboreshaji bora zaidi katika soka ya sasa - ni mabadiliko muhimu sana katika mchezo huu."
Didier Drogba alikuwa akizungumza na mwandishi wa BBC Sport Chris Bevan mjini Moscow.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.