Habari za Punde

Rais Dk Shein azungumza na Uongozi wa Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nd,Omar Hassan Omar (kulia) akisoama taarifa ya utekelezaji wa Mapngo kazi wa Mwaka 2017-2018  katika kikao Uongozi wa Wizara hiyo   kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwepo na Mshauri wa Rais  masuala ya Utamaduni na Utalii Mhe.Chimbeni Kheri Chimbeni(kushoto), [Picha na Ikulu.]29/06/2018.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 sambamba na Mpango kazi wa Mwaka 2018-2019, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]29/06/2018. 
 Mshauri wa Rais  Masuala ya Utamaduni na Utalii Mhe.Chimbeni Kheri Chimbeni(kulia)alipokuwa akichangia katika kikao cha Uongozi wa Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo cha  Utekelezaji wa Mpango kazi  wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018  kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwepo na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi Mhe,Mohamed Ramia Abdiwawa. [Picha na Ikulu.]29/06/2018. 
 Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Ali Abeid Karume (katikati) akisoma muhtasari wa Utekelezaji wa Mpango kazi  wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 katika kikao cha siku moja cha Uongozi kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe,Lulu Msham Abdalla(kushoto),[Picha na Ikulu.]29/06/2018. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.