Habari za Punde

Ulinzi Mkali Mkutano wa Rais Trump na Rais Kim: Uwezo wa walinzi 12 wa Kim Jong Un


Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore.
Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote .
Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka.
Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji.
Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri.
Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi.Mwisho-mlinzi mmoja huchunguzwa familia yake na vizazI vyake vilivyopita .
Maafisa wengi wa wapiganaji hao wana uhusiano na familia ya Kim Jong Un ama familia kubwa za Korea Kaskazini.
Wanapokubalika kuwa walinzi { huwezi kukataa kazi hiyo} hufanyiwa mafunzo ya kiwango cha juu .Walinzi hao hufunzwa kuwa na ujuzi maalum.Hufunzwa kwa kutumia bunduki, mbinu za uvamizi, judo, karate , kung fu na taekwndo .
Walinzi hao humzunguka kiongozi hiyo wakimlinda na wanaweza kuona kwa kuzunguka digree 360 kuwatazama watu walio karibu naye na walipo.Wanaotembea , mbele yake ni kati ya walinzi watatu hadi watano akiwemo mkurugenzi wa agfisia hiyo ya wapiganaji.
Pamoja naye , ni walinzi wanne hadi sita , wawili ama watatu wakiwa upande wake wa kulia Kuna wengine wanne ama watano nyuma yake.Ili kuonyesha uwezo wao katika utawala huo, ndio raia pekee wanaokubaliwa kubeba bunduki zilizo na risasi karibu na kiongozi wa taifa lao, sana sana huwa bunduki zinazodaiwa kuwa automatic pamoja na silaha nyengine.
Licha ya kubeba silaha, ulinzi mkubwa wanaompatia rais Kim jong un ni ujuzi walio nao katika kuwachunguza watu walio karibu na kiongozi huyo na kukabiliana na tishio lolote kwa kutumia mikono yao na mwili.
Wakati Kim Jong il alipokuwa hai mlinzi mmoja alikuwa akiwalinda maafisa wakuu wawili anaondamana nao.Walinzi wa Kim Jong Un ikilinganishwa na wale wa babake ni wachache na hawaonekani mara kwa mara. Walinzi hao huvalia suti za magharibi kama wanavyoonekana nchini Singapore .
Dereva wa Kim Jong un huvalia glavu za plastiki ama za ngozi kushika usukani. Pia hutumia mawasiliano ya redio kupitia hedifoni.Hatahivyo mbinu zao za mawasiliano ni za zamani.
Kitengo hicho cha afisi ya wapiganaji kina takriban kati ya maafisa 200-300, ambao nusu yao ni walinzi na waliosalia ni madereva na wafanyikazi wa kiufundi.Huku baadhi ya walinzi wa viongozi hao wakiwa watu walio na uzoefu mkubwa , wengi wao huwa wamefanya kazi kwa miaka 10.
Uchunguzi wa hivi karibuni na ripoti kuhusu ziara ya Kim nchini Singapore zimebaini kwamba ndege tatu ziliwasili katika mji mkuu wa Pyongyang .Walinzi wa Kim Jong un walikuwa ndani ya ndege hizo.
Wanaume hao na wanawake uhusishwa na usaidizi wa Kim. Wao husimamia laini za simu ambazo zitatumiwa na kiongozi huyo mbali na kumpatia tarakilishi yoyote anayotumia.
Mbali na hilo wana kinywaji , chakula na sigara zozote ambazo bwana Kim atataka kutumia wakati wa ziara yake Singapore na watachunguza chakula chochote ama kinywaji kabla ya kupakuliwa.Pia wana idara ya matibabu ambapo daktari wake wa maungo na maafisa wa matibabu na wawili kati ya maafisa hao wako naye ziarani Singapore.

Kuhusu ulinzi binafsi wa Kim, idara ya GC's #2 huweka ulinzi mkali wa karibu na huangazia pale bwana Kim anapofanya kazi , anapoishi na kutembea.
Iwapo unataka kuona eneo analokaa rais huyo katika hoteli ya St Regis nchini Singapore bila shaka utakutana nao.Ulinzi wa aina hiyo haiujawahi onekana kwengine kokote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.