Habari za Punde

Alisson: Liverpool yamfanya kipa wa Brazil kuwa ghali zaidi duniani

Liverpool imemfanya kipa wa Roma Alisson kuwa kipa ghali zaidi duniani baada ya kumsaini kwa kandarasi ya miaka sita.
The Reds hawajafichua kiwango cha fedha walicholipa kumpata raia huyo wa Brazil , lakini Roma imesema kuwa kandarasi hiyo iligharimu £66.8m (72.5m euros).
"Kulingana na maisha yangu na kazi yangu , hii ni hatua kubwa kwangu kuwa katika familia ya klabu hii '', alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Amekuwa katika klabu ya Roma kwa takriban miaka miwili , akishiriki mechi 37 za ligi ya Serie A mwaka 2017-18.
'Ni mmojwapo wa makipa wazuri zaidi duniani'
Mkufunzi wa Liverpool amesema kuwa usajili huo ni mzuri.
''Wakati mmoja katika wiki chache zilizopita , tulipata fursa ya kumsaini mmojwapo wa makipa waziuri duniani'' , aliongezea.
''Wenyewe walifurahi sana hivyobasi tukafanikiwa. hakuhusika katika kujadili thamani yake, walal pia sisi hatukuhusika. Ni soko na hivyo ndivyo ilivyo na hatutafikiria kuhusu hilo. Anafaa kuanza kuzoea ligi ya Uingereza . Ligi hii ni tofauti, marefa wako tofauti, maisha ya kipa yako tofauti katika ligi ya Premia''.
''Tulifanikiwa kumpata ili kuimarisha safu ya kipa ambayo ni muhimu sana''.
Alisson alisema kuwa uhamisho huo ulikuwa ndoto iliotimia na kufichua kwamba mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah ambaye alikuwa akicheza naye katika klabu ya Roma, alimtumia ujumbe kabla ya kukamilisha uhamisho huo.
Jana alinitumia ujumbe uliosema: Hey, unasubiri nini? wakati mazungumzo yalipokuwa yamepiga hatua kubwa, nilijibu mara moja nikisema: tulia niko njiani! nafurahia sana kuwa na fursa ya kucheza naye. Mbali na mchezaji mzuri, anatabia nzuri na mtu mzuri sana- ambacho ndio kitu muhimu zaidi.
Alisson ni mchezaji wa nne wa Liverpool kusainiwa tangu klabu hiyo imalize wa nne katika msimu wa ligi ya Uingereza wa 2017-18 na walishindwa na Real Madrid katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya.
Kiungo wa kati wa Brazil Fabinho, 24, alijiunga na klabu hiyo kutoka Monaco katika mkataba ambao una thamani ya worth more than £40m, huku kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 23, pia akijiunga na klabu hiyo kutoka klabu ya Ujerumani ya RB Leipzig katika dau la £48m deal..
Liverpool pia imemsaini mshambuliaji wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 26, kutoka klabu ya Stoke City.
Kuongezea, Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 26 ambaye aliifungia Liverpool mabao 44 katika mechi 52 aliandikisha mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo

Makipa walio ghali zaidi duniani Rekodi ya kipa ghali zaidi duniani ilikuwa ya Yuro 53 iliolipwa na Juventus kwa Parma kumnunua kipa Gianluigi Buffon mwaka 2001.

Rekodi ya kipa katika ligi ya Premia ni Yuro 40m ambazo klabu ya Manchester Zity iliilipa Benfica kumnunua Ederson mnamo mwezi Juni 2017.
Makubaliano hayo ya Buffon yalikuwa yenye thamani ya £32.6m wakati huo , huku Ederson akiwa na thamani ya £35m kutokana na mabadiliko ya viwango vya ubadilishanaji wa fedha , lakini makubaliano mengi kati ya klabu za Ulaya ikiwemo ile ya Uingereza hukamilishwa kwa Yuro hivyobasi rekodi ya Buffon ndio inayoongoza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.