Habari za Punde

Tetesi za soka Ulaya: Real Madrid, Willian, Hazard, Trippier, Neymar, Hart na Zaha

Real Madrid inajiandaa kuwasilisha ombi la £112m kwa Chelsea kumsaini mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 27. (Evening Standard)
Barcelona imewasilisha ombi la tatu kwa Chelsea kumsajili winga wa Brazil Willian, 29, wakitoa ombi la zaidi ya £55m. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas, 31, anasema kuwa anazungumza na Eden Hazard mara kwa mara ili kumzuia mchezaji huyo wa Chelsea kuhamia Real Madrid. (Telegraph)
Real pia huenda inataka kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa Tottenham Kieran Trippier kufuatia mchezo wake mzuri katika kombe la dunia akiichezea Uingereza..
Mabingwa hao wa Uhispania ni miongoni mwa orodha ya timu kadhaa za Uingereza na Ulaya zinazotaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sun)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26, amepinga madai kwamba anataka kuhamia Real Madrid huku klabu hiyo ikianzisha 'msako' wa mchezaji atakayemrithi Cristiano Ronaldo. (Marca)
Kipa wa klabu ya Manchester City Joe Hart huenda akaelekea Chelsea huku the Blues ikitaka kuwasilisha ombi la £5m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 (Sun)
Crystal Palace inataka kulipwa £70m ili kumuuza winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 25, ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na ananyatiwa na Everton na Borussia Dortmund. (Sun)
  • Everton imewasilisha ombi la £22m kumnunua beki wa Barcelona Lucas Digne,25 huku mkufunzi Marco Silva akiamini kwamba mchezaji huyo wa Ufaransa huenda akamrithi Leighton Baines katika klabu hiyo ya Goodison Park. (Mirror)
West Ham na Newcastle zimeanza mazungumzo na klabu ya Atlanta United ili kumnunua kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron, 24, kwa dau la £10m . (Sun)
West Brom itashindana na Middlesbrough na QPR ili kumsaini mshambuliaji wa Iceland Vidar Orn Kjartansson, 28, kutoka Maccabi Tel Aviv. (Birmingham Mail, via Mirror)
Winga wa West Brom James McLean yuko katika harakati za kujiunga na Stoke. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka taifa la jamhuri ya Ireland alifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya Ijumaa Friday. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Manchester City Oleksandr Zinchenko, 21, anasema kuwa anafurahi kuwa ,miongoni mwa timu ya Pep Guardiola licha ya Wolves kuwasilisha ombi la kitita cha £16m kumnunua raia huyo wa Ukrain.
Fulham na Newcastle pia zinamnyatia Zinchenko. (Express & Star)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.