Habari za Punde

Aston Villa: Nassef Sawiris bilionea Mwafrika anayewekeza klabu ya Aston Villa Uingereza

Wafanyibiashara mabilionea Wes Edens na Nassef Sawiris watawekeza kiwango kikubwa cha fedha katika klabu ya Aston Villa kulingana na klabu hiyo.
Raia wa Misri Sawiris anakadiriwa kuwa na thamani ya $6.8bn (£5.2bn), huku Mmarekani Edens ni mmiliki mwenza wa klabu ya mpira wa vikapu ya Milwaukee Bucks.
Mmiliki wa klabu ya Villa Dr. Tony Xia atakuwa mwenyekiti mwenza na kusalia kati bodi ya wakurugenzi.
Swala la kiwango cha fedha cha klabu ya Villa liliangaziwa baada ya klabu hiyo kukosa kupanda katika ligi ya Uingereza 
Villa ilioshushwa daraja mwaka 2016 , ilipoteza kwa Fulham mnamo mwezi Mei katika wuanja wa Wembley -na hivyobasi kupoteza fursa ya kurudi katika ligi ya Uingereza abapo wangepata zaidi ya £160m.
Klabu hiyo ilikosa kulipa kodi ya £4m mwezi Juni huku Xia akidaiwa kuwa na tatizo la kifedha kutokana na sheria kali za fedha zinazotoka China. Hathivyo Villa iliweza kulipa deni hilo baadaye.
Je wawekjezaji hawa wa Villa ni akina nani?
Jarida la Forbes linakadiria kwamba Sawarris mwenye umri wa miaka, 57, ana thamnai ya $6.8bn (£5.2bn) akiwa miongoni mwa familia tajiri nchini Misri-babake na nduguze pia wakiwa mabilionea.
Wafanyibiashara hao waliokita kambi mjini London wanamiliki OCI - mojwapo wa kampuni kubwa ya mbolea pamoja na kampuni ya ujenzi ya Orascom .
Baada ya kufanya kazi kuhusu maswala ya kifedha, Edens mwenye umri wa miaka , 56, alianzisha kampuni ya uwekezaji ya Fortress Investment Group mwaka1998.
Aliiuza mwezi Januari kwa takriban $3.3bn kwa kampuni ya Japan, iliomfanyia kutia kibindoni $500m, na kuinunua Milwaukee Bucks kwa $550m mwaka 2014 pamoja na mfanyibiashara mwenza Marc Lasry.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.