Na Abdi Suleiman -Pemba.
Timu ya New
Star ya Wete hatimae imefanikiwa kutwaa
ubingwa wa Tamasha la Utalii,
Utamaduni, Biashara na
Michezo Pemba, baada ya kuifunga Timu ya Mwenge kwa
mikwaju ya Penant 3-2.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa michezo Gombani,
huku
ukihudhuriwa na mashabiki wengi wa soka uwanjani
hapo, awali timu hizo
zilimaliza dakika 90 zikiwa
zimefungana bao 1-1.
Fainali hiyo iliyowakutanisha watoto wa Mjini wete, iliweza
kuvuja hisia za mashabiki wa soka, kutaka kuiyoa Mwenge
itaendelea kuwa mteja
wa New Star, kwani timu hiyo imekua
ikizisumbua Jamhuri na Mwenge kila
zinapokutana.
Kumalizika kwa mchezo huo Kocha wa Timu ya New Star,
Ustadhi Yahya Ali alisema ushindi huo umetokana na
wachezaji wake kukubalia kucheza mpira na kuepuka kiingia aibu ya kufungwa na Mwenge.
Alisema mwenge ni timu Kubwa na katika Wete, hivyo
ataendelea
kuiheshimu kila watakapokutana lakini
wasitegemee kuifunga New Star kila
watakapokutana.
No comments:
Post a Comment