Na.Abdi Suleiman -Pemba.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Taasisi ya Viwango Zanzibar
Khatib Mwadini Khatib, amewataka wanamichezo
Kisiwani
Pemba kuhakikisha wanakula na kutumia vifaa vya michezo,
ambavyo vimechunguzwa
na Taasisi ya Viwango Zanzibar ili
kulinda afya zao.
Alisema pindi wanamichezo wakitumia vitu ambavyo
vimechunguzwa
na Taasisi hiyo, wataweza kuepukana na
maradhi mbali mbali yataweza kuua
viwango vyao.
Mkurugenzi huyo alitoa kauli hiyo wakati wa kukabidhi
zawadi kwa
washindi wa marathoni katika Viwanja vya
michezo Gombani, ikiwa ni tamasha la
Utalii, Utamaduni,
Biashara na Michezo Pemba.
Alisema serikali imekuwa ikiwategemea wanamichezo katika
kuutangaza utalii wake ndani na nje ya nchi, wanamichezo
wananafasi kubwa ya
kutumia vyakula ambavyo
vimepitishwa na taasisi ya ZBS.
“Siku hizi kumekua na bidhaa mbali mbali zinaingia nchini
ikiwemo vitu vya mitumba, vizuri wanamichezo kutumia vitu
ambavyo vimepitishwa
na taasisi yetu ya viwango Zanzibar,
ili kulinda afya zetu kutokana na umuhimu
wetu katika
nchi”alisema.
Alisema serikali imekua mstari wa mbele katika kuinua
michezo,
haipendezi leo kuona wachezaji wanashindwa
kufikia malengo yao kutokana na
kutumia vifaa na kula
chakula ambacho hakina kiwango.
Hata hivyo aliwapongeza wanamichezo wote walioshiriki
katika
mashindano ya Marathoni, ikizingatiwa michezo ni
ajira, udungu, urafiki na
afya.
No comments:
Post a Comment