Habari za Punde

NAIBU WAZIRI AWESO AAGIZA ALIYEKUWA KUWA MHANDISI MAJI LUSHOTO ALIYEHAMISHIWA MASWA KUPELEKA MIKATABA YA MAJI SHUME WIZARANI NDANI YA WIKI MOJA


NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akifuatilia kwa umakini mkataba wa Maji wa Shume kuangalia mapungufu yaliyopo jana kabla ya kupelekwa Wizarani katikati ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Karim Lichela kushoto ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Tang Uwasa Rashidi Selemani
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akifuatilia kwa umakini mkataba wa Maji wa Shume kuangalia mapungufu yaliyopo jana kabla ya kupelekwa Wizarani katikati ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Karim Lichela kushoto ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Tang Uwasa Rashidi Selemani wa mwisho kushoto ni Mhandisi wa Maji Mkoa wa Tanga Ladislaus Modestus

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa tatu kutoka kushoto akimsikiliza Katibu Tawala wa wilaya ya Lushoto wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Ngulu kata ya Magamba wilayanu lushoto wakati wa ziara yake

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua tenki la Maji la Kata ya Kwamashai wilayani Lushoto wakati wa ziara yake.

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameagiza aliyekuwa Mhandisi wa Maji wilaya ya Lushoto ambaye amehamishiwa Maswa mkoani Shinyanga afike wilayani humo kuchukua mikataba ya mradi wa maji Shume ndani ya wiki moja aupeleke wizarani.

Mradi huo wa ujenzi wa miundombinu ya maji Shume Manola  hadi Madala unatakelezwa na mkandarasi MS Organes Contractors Co.Limited wa wilayani Lushoto ambapo unagharimu kiasi cha Bilioni 2,493,272,852.

Aweso alitoa agizo hilo jana wakati akihitimisha ziara yake wilayani Lushoto ambapo aligundua kuwepo kwa mkanganyika kwa ulipwaji wa fedha za mradi wa Maji shume ambazo zimepelekwa na serikali kwa kulipwa mkandarasi kwa kiwango tofauti kwenye mkataba mmoja.

Fedha ambazo alibaini kulipwa mkandarasi huyo  kwa certificate ya kwanza mkandarasi alipaswa kulipwa kiasi cha bilioni 2.4,ya pili mkatandas alilipwa bilioni 2.4 na tatu inaonyesha alilipwa kiasi cha bilioni 2.9 jambo ambalo liliibua sintofahamu wakati wa kikao hicho baada ya kushindwa kupata maelezo halisi.

“Ndugu zangu haiwezekani mradi mmoja unakua gharama tatu tofauti ambazo zina tofautiana na ndio sababu nimelazimika kuagiza mikataba yote irudi wizara kwenda kuhakikiwa kwa lengo la kuweza kubaini gharama halisi ya mradi “Alisema

Naibu Waziri huyo alisema kutokana na kuwepo kwa dalili za ubadhirifu  ndani ya mradi huo wizara haitaweza kutoa fedha katika mradi huo hadi pale wataalamu kutoka wizarani kuufanyia uchunguzi mradi huo .

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wizara itaunda tume ili kuchunguza miradi hiyo ya maji nchi nzima huku akiwataka wahandisi wa maji kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji safi na salama kwenye maeneo yao.

“Lakini niseme kwamba kama kuna certificate inayotakiwa kulipwa sasa hivi nitawasiliana na katibu mkuu ili malipo hayo yasitishwe hadi uhakiki utakapo kamilika hasa kwa kipindi hiki kifupi ambacho wizara na wataalamu wake wanauhakiki mradi huo”Alisema

Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia alisema anaishukuru serikali kwa kutekeleza miradi kwenye Jimbo lake kutokana na kwamba changamoto ya maji imekuwa kikwazo kikubwa sana kwa wananchi wake.

Aidha alimuomba Naibu Waziri huyo kuiangalia Jimbo hilo kwa ukaribu zaidi ili kuweza kuwasaidia wananchi waweze kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma ya maji jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.