Habari za Punde

Tanzia ya Mpiga Picha wa Zamani wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo Tanzani.

TANZIA: Mpiga picha wa zamani wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Mzee Mwalimu Omari amefariki dunia leo. Msuba upo nyumbani kwa marehemu Mburahati jijini Dar. Taarifa zinasema kwamba mazishi yamepangwa kufanyika kesho huko huko Mburahati.
Huu ni msiba mzito kwetu sisi tuliobahatika kupita kwenye mikono ya Mzee Mwalimu Omari na wenzie kina Adinani Mihanji, Vicent Urio, Sam Mmbando, Ernest Millinga na Jonas Mwasumbi ambao nao wametangulia mbele ya haki.
Mola ailaze pema roho ya marehemu, AMINA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.