Habari za Punde

Mwanamke wa Kwanza Nchini Japan Luteni Misa Matsushima Kuendesha Ndege ya Kivita Japan

Mwanamke wa kwanza Nchini Japan kurusha ndege ya Kivita Misa Matsushima,akiwa katika moja ya ndege za kivita katika moja ya Uwanja wa Ndege Nchini Japan. 

Mwanamume raia wa Japan ataendesha ndege ya kivita ya nchi hiyo na kuwa mwanamke wa kwanza kufanya hivyo nchini humo.
Luteni Misa Matsushima, 26, ataanza kazi yake siku ya Ijumaa baada ya kukamilisha mafunzo ya kuendesha ndege aina ya F-35 kwa mujibu wa jeshi la Japan.
"Kama mwanamke wa kwanza rubani wa ndege ya kivita, nitafungua njia," aliwaaambia waandishi wa habari.
"Tangu nione filamu ya Top Gun nikiwa shule ya msingi, nimekuwa nikitaka niwe rubani wa ndege za vita," mwanafunzi huyo wa zamani wa taasisi ya ulinzi ya Japan aliwaambia waandishi wa habari.
Ninataka kufanya kazi kwa bidii kutumia ndoto yangu - sio tu kwangu binfasi bali kwa wanawake wengine kufuata siku za usoni.
Wanawake wengine watatu wanapata mafunzo ya kujiunga na kundi la marubani.
Luteni Misa Matsushima, akiwa kazi Nchini Japan. 
Ndege za F-15J ambazo wataendesha ni zile zina injini mbili ambazo zinatengenezwa kupambana na ndege zingine hewani. Zinaweza kufka kasi ya ya mara mbili unusu au 2.5 ya ile ya sauti karibu kilomita 3000 kwa sasa.
Rubani huyo mwenye miak 26 alikuwa na mpango wa kuendesha ndege za usafiri za jeshi kabla ya kuondolewa marufuku hiyo.
Japan ina viwango vya juu vya kutokuwepo usawa wa kijinsia huku wanawake wakitajwa kuwa wa nyumbani badala ya kufanya kazi.
Lakini kutokana na sababu kuwa watu wengi wanazidi kuzeeka na ukosefu wa wafanya kazi, waziri mkuu shinzo Abe aliahidi mwaka 2013 kuwapa nguvu wanawake.
Mapema mwaka huu Ryoko Azuma alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza meli ya kijeshi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.