Habari za Punde

Rais Dk Shein akutana na Gavana wa Bali nchini Indonesia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bw.James Coasta,C.H.A. Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Discovery Kartika Plaza iliyopo katika Mji wa Bali Nchini Indonesia mara baada ya kuwasili katika Mji huo akiwa na ujumbe wake katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.  

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine katika ujumbe wake wakiangalia ngoma za kiutamaduni Mjini Bali nchini Indinesia baada ya mapokezi katika   Hoteli ya Discovery Kartika Plaza,katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.  
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Gavana wa Mji wa Bali nchini Indonesia Bw.IMade Mangku Pastka kwa mazungumzo katika Hoteli ya Discovery  Kartika Plaza alipokuwa katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwatambulisha Viongozi  aliofuatana nao katika ziara ya kikazi alipotembelea Mji wa Bali kwa Gavana wa Mji huo Bw. IMade Mangku Pastka kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Hoteli ya Discovery  Kartika Plaza  ziara hiyo ni  mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchini Indonesia Mhe. Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Gavana wa Mji wa Bali nchini Indonesia Bw.IMade Mangku Pastka (katikati) wakiwa katika  mazungumzo ya pamoja na Viongozi wengine wa pande zote mbili katika Hoteli ya Discovery  Kartika Plaza,Rais alipokuwa katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yao na  Gavana wa Mji wa Bali nchini Indonesia Bw.IMade Mangku Pastka yaliyofanyika jana  katika Hoteli ya Discovery  Kartika Plaza akiwa katika ziara ya kikazi na Ujumbe aliofuatana nao Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE
Bali, Indonesia                                                                04.08.2018
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza fursa iliyotolewa na uongozi wa Serikali wa kisiwa cha Bali ya kwenda kujifunza uendeshaji wa sekta ya Utalii hasa ikizingatiwa kuwa Bali imepata mafanikio makubwa katika sekta hiyo.

Dk. Shein aliyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Jimbo la Bali (Gavana) I Made Mangku Pastka, mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kartika Plaza iliyopo mjini Bali.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa fursa hiyo ni ya pekee na inajenga imani kubwa kwa Zanzibar kutokana na uhusiano wa kihistoria uliopo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar na Indonesia.

Alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa fursa kwa wanafunzi wa kada ya utalii wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kupata nafasi ya kwenda kujifunza namna ya uendeshaji wa utalii katika kisiwa hicho ambacho kimepata mafanikio makubwa kutokana na sekta ya utalii kuimarika.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa kiongozi huyo kwa mapokezi na makaribisho yake makubwa aliyomfanyia yeye na ujumbe wake katika kisiwa hicho kiliopo Kusini Mashariki mwa Jakarta.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa kipindi kirefu Zanzibar imeingia katika shughuli za kitalii ikiwa na lengo la kukuza uchumi na kuinua pato la Taifa ambapo kwa hivi sasa sekta hiyo imekuwa ikichangia fedha za kigeni kwa asilimia 80.

Alieleza kuwa miongoni mwa malengo katika kukuza sekta hiyo kwa upande wa Zanzibar ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar iweze kupindukia lengo lililokusudiwa la kufikia watalii laki tano kwa mwaka.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza haja ya Zanzibar kushirikiana na Bali katika kuendeleza sekta ya uvuvi ambayo nayo imeweza kupata mafanikio makubwa katika kisiwa hicho.

Mapema katika maelezo yake Kiongozi Mkuu huyo wa Bali alimkaribisha Rais Dk. Shein kiswani hapo na kumueleza jinsi yeye mwenyewe binafsi pamoja na wananchi wa kisiwa hicho walivyofarajika kutokana na ujio wa Rais Dk. Shein hatua ambayo inazidi kujenga uhusiano uliopo kati ya Indonesia na Zanzibar.

Alieleza kuwa kutokana na shughuli kubwa za kisiwa hicho kuwa ni za kitalii na kupelekea kuwa na hoteli nyingi za kitalii, vyuo vya kitalii pamoja na kuwepo huduma mbali mbali zinazotolewa kwa watalii hivyo alimueleza Dk. Shein Zanzibar kuwa wako tayari kutoa nafasi za kwenda kujifunza huko Bali ili Zanzibar nayo izidi kuimarika katika sekta hiyo.

Aliongeza kuwa Bali iko tayari kutoa nafasi za masomo kwa vijana wa Zanzibar wa kada ya utalii kwenda kujifunza zaidi kisiwani humo na hata kwenda kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na utaalamu.

Pia, kiongozi huyo alimueleza Rais Dk. Shein mafanikio iliyoyapata Bali katika kuimarisha sekta ya uvuvi na kuunga mkono kuwepo kwa mashirikiano baina ya pande mbili hizo.

Akiwa katika ukumbi wa hoteli ya Kartika Plaza iliyopo mjini Bali, Rais Dk. Shein alikutana na uongozi wa Kampuni ya Utalii ya Bali ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Abdulbakar Mansoer ambaye alieleza mafanikio yaliopatikana katika sekta ya utalii kisiwani humo huku akiahidi mashirikiano kati ya Bali na Zanzibar.

Wakati huo huo Dk Shein alitembelea Chuo Kikuu cha Udayana kiliopo Jambaran mjini Bali na kupata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Chuo hicho pamoja na wananfunzi wa chuo hicho katika ukumbi wa jengo la uongozi wa chuo hicho wa Ruang Bangsa.

Akizungumza na uongozi wa Chuo hicho Rais Dk. Shein alitoa pongezi na shukurani kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Udayana kwa mapokezi mazuri waliyomfanyia yye na ujumbe wake pamoja na kusisitiza haja ya kuwepo kwa mashirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na chuo hicho.

Nao uongozi wa Chuo Kikuu cha Udayana walieleza kufarajika kwao na ziara hiyo ya Dk. Shein katika Chuo Chao hicho na kueleza kuwa imefungua ukurasa mpya wa mashirikiano kati ya Zanzibar na Bali hasa ikizingatiwa kuwa miongoni mwa masomo makuu ya Chuo hicho ni masomo ya Utalii ambapo tayari Chuo Kikuu cha SUZA nacho kimeshaanzisha kada.

Akizungumza na wananfunzi katika ukumbu wa Ruang Bangsa Chuo hapo Rais Dk. Shein aliwasisitiza kusoma kwa bidii na maarifa hasa ikizingatiwa kuwa nchi yao ya Indonesia inawategemea kuwa viongozi na watendaji wazuri wa hapo baadae.

Dk. Shein ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), aliwakaribisha wanafunzi hao kuja Zanzibar kujifunza, kutembelea pamoja na kubadilishana uzoefu na utaalamu na Chuo Kikuu cha SUZA.

Rais Dk. Shein pia, alikubali wazo la Chuo Kikuu cha SUZA cha Zanzibar kuwa na mahusiano na Chuo hicho kama ilivyoombwa na uongozi wa chuo hicho na kusisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizo.

Dk. Shein pia, aliwaeleza historia ya Zanzibar jinsi ilivyoingia katika sekta nzima ya biashara pamoja na utalii ambao ni sehemu ya maisha kama ilivyo kwa Indonesia ambapo alieleza kuwa utalii wa Zanzibar uliimarishwa zaidi mara baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 ambapo sekta hiyo iliwekewa mikakati maalum.

Aidha, Rais Dk. Shein alaieleza kuwa ukongwe wa Chuo hicho ambacho kimeanzishwa miaka 56 iliyopita uzoefu wake utakuwa msaada mkubwa kwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) iwapo kutakuwa na mashirikiano ya pamoja.

Mara baada ya kumaliza ziara katika Chuo Kikuu hicho cha Udayana, Rais Dk. Shein alitembelea ofisi ya  Kampuni ya mafuta ya nazi ya ‘Samani Island Virgin Coconut Oil’ ambapo uongozi wa Kampuni hiyo ulimueleza shughuli inazozifanya pamoja na mafanikio uliyoyapata kutokana na kuwa na soko la uhakika la mafuta ya nazi la ndni na nje ya nchi ikiwemo Ujerumani,Australia, Bulgaria, Japan na nchi nyenginezo.

Kwa maelezo ya Rais Dk. Shein lengo kuu la ziara hiyo katika Ofisi hizo ni kuangalia uwezekano wa kushirikiana pamoja kampuni hiyo katika kufufua biashara pamoja na kilimo cha nazi ambacho kiliijengea sifa kubwa Zanzibar hapo siku za nyuma 

Rais Dk. Shein akiwa katika kisiwa hicho cha Bali aliungana na Waislamu ambao ni asilimia kubwa ya wakaazi nchini Indonesia pamoja na kiswa hicho katika sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Huda Islamiya Mjini Bali.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.