Habari za Punde

Tamasha la Eid Katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja Lafana Katika Viwanja Hivyo na Kuwa Kivutio Kwa Watoto Waliofika Katika Viwanja Vya Sikukuu.

Watoto wakiwa katika viwanja vya Sikukuu Mnazi Moja wakifuatilia Tamasha la Eid lililofanyika katika viwanja hivyo kwa burudani mbalimbali za ngoma za Asili na Zenj Flava na Wasanii wa Vichekesho. Tamasha hilo limavuta hisia za Watoto wengi waliofika katika viwanja hivyo kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Hajj.
Watoto wakionesha jisi ya kulisakata rumba wakati wa Tamasha la Eid katika Viwanja vya Sikukuu vya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Kikundi cha Madensa cha DreanDance wakitowa burudani katika Onesho la Tamasha la Eid Al Hajj katika viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.


Wasanii wa Kikundi cha Chekanao Mwanakwerekwe Zanzibar wakionesha umahiri wa kucheza Ngoma ya Kibati wakati wa Onesho la Tamasha la Eid katika Viwanja vya Sikukuu Vya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Msanii wa uigizaji wa Sauti za Wanya mbalimbali akionesha uhodari wake wa kuigiza sauti mbalimbali wakati wa Tamasha hilo la Eid Al Hajj katika viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Msanii wa Kizazi Kipya Zanzibar Imma ikionesha umahiri wake wakati wa Tamasha la Eid Al Hajj katika viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar. 
Msanii Rico Singo akitowa burudani wakati wa Onesho la Tamasha la Eid Al Hajj katika viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.