Habari za Punde

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania NEC Yakabidhiwa Jengo la Ofisi Maisara Zanzibar.

 Picha ya jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mjini Zanzibar. Jengo hilo limetolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia akifafanua jambo kwa  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Salum Kassim Ali (kulia), Mkuu wa Idara ya Utawala ya NEC Bw. Hamis Mkunga (kushoto), Mkuu wa Idara ya Habari ya NEC, Bi. Giveness Aswile (wa pili kutoka kulia) na Mkuu wa Idara ya Manunuzi ya NEC Bw. Eliud Njaila mara baada kukabidhiwa jengo la Ofisi litakalotumiwa na NEC mjini Zanzibar jana.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia (kulia) akizungumza na Watendaji wa Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) jana mjini Zanzibar mara baada ya watendaji hao kukabidhi jengo la Ofisi litakalotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar. Jengo hilo ambalo liko chini ya Shirika la Bandari Zanzibar limetolewa kwa NEC na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia akiangalia mandhari ya nje ya jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lililotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wengine pichani ni baadhi ya Watendaji wa Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) ambalo jengo hilo lilikua chini yao.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akizungumza na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Shirika la Bandari Zanzibar mjini Zanzibar wakati wa Makabidhiano ya jengo la Ofisi litakalotumiwa na NEC Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia akikagua sehemu za nje za jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lililotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Salum Kassim Ali (kulia), akifafanua jambo kwa  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Athumani Kihamia (wa pili kutoka kulia) na watendaji wengine wa NEC jana mjini Zanzibar.
Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Shirika la Bandari Zanzibar wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Shirika hilo Bw. Mrisho Haji Mrisho jana mjini Zanzibar
(Picha na NEC Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.