Habari za Punde

Wananchi waridhia bwawa la Urughu kutangazwa kama eneo lindwa-kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi waishio pembezoni mwa ziwa Kitangiri Wilayani Igunga. Waziri Makamba amewaasa wakazi hao kuwa chachu katika kuhifadhi mazingira ya ziwa hilo kwa manufaa ya sasa na baadae.

Wakazi wa mwalo wa Shauri-Tanga katika Ziwa Kitangiri Wilayani Iramba, wakizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba juu ya namna wanavyotumia ziwa hilo kwa shughuli za uvuvi.

Bwawa la Urughu lilipo Wilayani Singida liko hatarini kutoweka kutokana na matumizi yasiyoendelevu ya shughuli za kibinadamu yanayopelekea kujaa mchanga na  kupungua kwa kina cha maji. Waziri Makamba ameazimia kutangaza bwawa hilo kama eneo lindwa kimazingira ili kuweka ulinzi na matumizi endelevu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.