Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu Akizungumzia Kukamilika Kwa Maandalizi ya Kongamano la Tano la Diaspora Kisiwani Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Gagu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Serikali na binafsi kuhusiana na kukamilika kwa Maandalizi ya Kongamano la Tano la Diaspora Zanzibar. Kwa Mwaka huu litafanyika kisiwani Pemba kuazia tarehe 18 na 19 mwizi wa Agusti 2018. Linategemewa kushiriki Wanadiaspora kutoka Nchini mbalimbali wenye Asili ya Zanzibar na Tanzania Bara. 
Kongamano hilo litaazia katika Meli ya Mapinduzi 2 wakati wa safari ya kuelekea Kisiwani Pemba kwa kutolewa burudani za muziki wa Asali ya Zanzibar na maonesho mbalimbali ya Maendeleo. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mdogo wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gagu akizungumza na Waandishi wa habari na kusisitiza jambo wakati wa mkutano wake wa kutoa taarifa ya Mkutano wa Kongamano la Tano la Diaspora Zanzibar litakalofanyika Kisiwani Pemba Wiki Ijayo.
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa kina mkutano wao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji gavu wakati akitowa taarifa ya kukamilika kwa Kongamano la Tano la Diaspora Zanzibar litakalofanyika Kisiwani Pemba Wiki ijayo.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.