ISO
9001: 2015 CERTIFIED
IDARA YA FORODHA NA USHURU WA BIDHAA
TAARIFA KWA UMMA
UTOAJI WA TAARIFA KUHUSU FEDHA TASLIMU NA
HATI ZA MALIPO ZINAZOSAFIRISHWA KUINGIA NCHINI AU KUTOKA NJE YA NCHI
Taarifa inatolewa kwa umma kwamba Sheria namba
10 ya
mwaka 2009 inayohusu utakatishaji wa fedha haramu na
kanuni yake ya mwaka
2015 imeipa uwezo ofisi ya Zanzibar
ya TRA kusimamia kazi ya kupokea taarifa
zinazohusu
usafirishaji wa fedha na Hati za malipo zinazoingia nchini na
kusafirishwa nje ya nchi.
Taarifa
hii inahusu usafirishaji wa fedha taslimu au hati za malipo (Bearer Negotiable
Instruments) zinazofikia au kuzidi dola za kimarekani elfu kumi (USD10,000) au
fedha nyingine yoyote yenye thamani sawa na hiyo, iwapo fedha au hati hizo zitasafirishwa
kwa njia zifuatazo
(a)
mtu yeyote anayesafiri akiwa nazo au katika
mizigo anayoambatana nayo
au
katika chombo cha usafiri;
(b) katika makontena ya kubebea
mizigo, na
(c) kwa njia ya vifurushi.
Kutokana
na uwezo iliyopewa kisheria, ofisi ya Zanzibar ya
TRA inachukua fursa hii
kuutaarifu umma kuwa, kuanzia
tarehe 13 Agasti 2018, mtu yeyote atakaesafirisha
fedha
taslimu au hati za malipo zinazofikia kiwango kilichotajwa
na kanuni hizi
atalazimika kutoa taarifa wakati wa kusafirisha kwa kujaza fomu maalum zitakazopatikana
kwa maafisa forodha waliopo uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, Bandari ya Malindi,
Bandari ya Mkoani, Bandari ya Wete na uwanja ndege wa Pemba.
Wananchi wote wanajulishwa kuwa kutotoa
taarifa
au kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu usafirishaji
huo ni kosa kisheria
Kwa
taarifa au ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na TRA-Zanzibar kwa namba za
simu 0242232923,0242232837/8 au Barua pepe: trazanzibar@tra.go.tz
Ifahamike
kuwa, utaratibu huu haukusudii kuzuia
usafirishaji wa fedha taslimu na hati za
malipo
kuingia au kutoka nchini.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
IMETOLEWA
NA:
NAIBU
KAMISHNA
TRA-ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment