Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mhe.Raya Issa Msellem akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kukamilika Kwa matayarisho ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Tisa, unaotarajiwa kufanyika wiki hii na kuwasilisha miswada ya Sheria Mitatu na kuwasilisha na Majibu 154 na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Miswada ya Sheria inayotarajiwa kuwasilishwa na Kusomwa Kwa mara ya Kwanza katika Mkutano wa mwezi wa Mei,2018 itakayosomwa katika Mkutano huu wa Kumi na Moja unaotarajiwa kufanyika tarehe19 September 2018.
i) Miswada wa Sheria Kuweka Masharti Bora ya Usimamizi wa Mahakama,Kufafanua Utumishi wa Mahakama,Kuazisha Ofisi za Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Mrajis,Kuazisha Mfuko waMahakama na kuweka Mashartimengine yanayohusiana na hayo.
ii)Mswada wa Sheria ya Kuazisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu na kuweka Masharti ya ukaguzi wa Elimu pamoja na Mambo mengine yanayohusiana na hayo.
iii) Mswada wa Sheria ya Kuazisha Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar na kuweka Masharti Bora yanayohusiana na kazi,uwezo,uongozi na Mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Raya Issa Msellem akizungumza na waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali na Binafsi Zanzibar akitowa taarifa ya Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar linalotarajiwa kuaza wiki hii. tarehe 19-9-2018.
Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Zanzibar wakifuatilia Taarifa ya Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar linalotarajiwa kuaza Jumatano wiki hii. katika ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndh Himid Choko akitowa maelezo baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa kutowa Taarifa ya Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar.
Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Zanzibar wakifuatilia Taarifa ya Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar linalotarajiwa kuaza Jumatano wiki hii. katika ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment