Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Kuaza Ziara Yake ya Siku Nne Mkoani Kigoma.

Na. Mwandishi OMR.                                                                                                     
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 8 Septemba, 2018 anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo mkoani Kigoma kwa siku nne.
Mara atakapowasili mkoani Kigoma atapokea Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa. Aidha, tarehe 9 Septemba, Makamu wa Rais atashiriki katika Sherehe za kuwekwa Wakfu Askofu Mkuu Msaidizi na Maaskofu wengine wanne wa majimbo katika kanisa la Pentekoste Motomoto Mwanga.
Tarehe 10, Makamu wa Rais atatembelea mwalo wa Muyobozi, atakagua ujenzi wa kituo cha Afya Uvinza na kuhutubia wananchi katika kijiji cha Kazuramimba.
Makamu wa Rais atahitimisha ziara yake tarehe 11, kwa kutembelea Wilaya ya Buhigwe ambapo pamoja na mambo mengine atazungumza na Wananchi wa Buhigwe katika eneo la Munzeze.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.