Habari za Punde

NITAENDELEA KULINDA NIDHAMU KWENYE VIKAO VYA BARAZA LA MADIWANI-MEYA TANGA SELEBOSIMSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Selebosi Mustapha akizungumza katika Kikao cha Baraza la Madiwani
 MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mustapha Selebosi
 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza katika kikao hicho
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi kulia akisistiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Naibu Meya Mohamed Haniu
 NAIBU Meya wa Jiji la Tanga Mohamed Haniu akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi
 Sehemu ya baadhi ya madiwani wakifuatilia kikao hicho
 Sehemu ya Madiwani wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho
 Madiwani wakifuatilia hoja mbalimbali
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mustafa Seleboss amesema atahakikisha anaendelea kulinda nidhamu ndani ya vikao vya baraza la madiwani ili kutoa mwanya kwa madiwani kujadili kwa kina maslahi ya wananchi badala ya kuingiza itikadi za kisiasa.

Hayo ameyazungumza mbele ya waandishi wa habari baada ya kumalizika kikao hicho cha kufunga mwaka baada ya madiwani wanne toka chama cha wananchi [CUF] kuruhusiwa kuingia katika baraza hilo kutokana na kusimamishwa kutokushiriki vikao hivyo kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Aidha alisema mbali ya kuweka mbele maazimio ya kikao hicho cha kufunga mwaka 2017/2018 na kuelekea kuanza mwaka wa 2018/2019 bado alisisitiza swala la nidhamu ndani ya mijadala ya vikao hivyo ili
ilete tija kama azma ya madiwani wote ya kupeleka maendeleo katika kata zao.

Seleboss alisema madiwani hao walisimamishwa kwa mujibu wa kanuni hivyo kutokuwepo ndani ya vikao kadhaa iwe fundisho kwao na wengine kutokana na kutokushiriki vema katika jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wao.

“Hatufanyi kazi kwa kumuonea mtu bali tunaangalia kanuni ndizo zinazotuongoza hivyo madiwani wenzangu tuunganeni kwa pamoja katika harakati za kusukuma maendeleo katika kata zetu ……na niweke wazi humu
ndani tulumbane kwa hoja na sio siasa”Aalisema Seleboss.

Katika hatua nyingine Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tanga Ruth Mkisi aliwaapisha madiwani wawili Omari Mzee kata ya Makorora na Jumaa Ramadhani kata ya Mabokweni ambao walishinda katika uchaguzi mdogo uliomalizika Agosti 12.

Kwa uapande wake Diwani wa kata ya Duga Khalid Rashid alisema ni wakati wa kwenda kuwawakilisha wananchi wake katika baraza hilo kiukamilifu ili kuweza kufikisha kero zao na kuwaletea maendeleo.

Rashid alisema walizuiliwa kwa kutokuhudhuria vikao vitatu kwa mujibu wa Meya jambo ambalo liliwalazimu kukaa nje ya baraza hilo takriban mwaka mmoja huku wakishindwa kufikisha kero za wananchi wao.

“Tuliambiwa tumepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vitatu lakini tulikaa nje ya baraza hili mwaka mmoja sasa tangu Agosti 31 mwaka jana lakini nashukuru tumerudi wakati umewadia wa kuwatetea wananchi wa
kata yangu na kupigania maendeleo yetu”Alisema Rashid.

Nae Diwani wa kata ya Msambweni Abdurahman Hassan alisema wamerejea kwenye kikao hicho na si muda wa kumtafuta mchawi huku jambo la msingi kuangalia maendeleo ya kata hiyo na kuwawakilisha wananchi wake vizuri katika baraza hilo.

Madiwani ambao walisimamishwa ni pamoja na Abdurahman Hassan kata ya Msambweni,Khalid Rashid kata ya Duga,Seleman Mbaruku kata Majengo,mwasaju Juma kata ya Mabawa na Rashid Jumbe ambae hakuwezakufika kutokana na kuwa na kesi mahakamani ya kuvuliwa uwanachama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.