Habari za Punde

'Ukimwi bado ni tishio'

Na Mwashungi Tahir        Maelezo     29-9-2018.
NAIBU  Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Mohamed Ahmada Salum amesema ukimwi ni tishio kubwa kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani hivyo tupige vita kwa nguvu zote kuhakikisha suala hili lisiendelee.
Hayo ameyasema leo huko huko katika ukumbi wa jengo la Mtakwimu wakati alipokuwa akifungua semina ya viongozi ya kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na virusi vya homa ya ini.
Amesema kutokana na tishio ya maradhi haya jamii isiyabeze bali tuweke nguvu zetu kwa kuyapiga vita ili maambukizi mapya yasizidi kujitokeza , kwani Zanzibar ukimwi upo  maeneo tofauti ambapo kwa mkoa wa Mjini Magharibi unaongoza kwa asilimia 0.4 .
Aidha  alisema  juhudi na maarifa  yanahitajika katika kuhakikisha Taifa lenye nguvu linatokana na watu wenye afya  na kuhakikisha ifikapo 2030 maambukizi mapya yanamalizika.
Nae msoma risala  Hamida Ubwa Mamboya wa Kamati ya ukimwi na Jinsia ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege alisema elimu inaendelea kutolewa wa wafanyakazi ambayo ni katika  majukumu ya uhamasishaji wa kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi mahala pa kazi na kushajihisha wafanyakazi kupima afya zao mara kwa mara kwa lengo la kujitambua.
Semina hiyo ya siku moja imeandaliwa na kamati ya ukimwi na jinsia juu ya mamlaka ya viwanja vya ndege na kujadiliwa mada nne  ikiwemo thamani, elimu na Athari za virusi vya ukimwi na vya homa ya ini, ushuhuda na ngono ya rushwa.
Mwisho
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.