Habari za Punde

WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VYOMBO VYA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA AFRIKA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa 28 wa Wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya Kanda ya Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam leo Kamishna wa Uhuduma wa  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Valite Mwashusa amesema mkutano huo utaanza Septemba 17 hadi Septemba 21 mwaka huu.

Amefafanua utafanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam na lengo ni kubadilisha uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

"Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na dawa za kulevya na vitendo vya uhalifu itaratibu mkutano huo," amesema Mwashusa.

Amesisitiza mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na sababu za mkutano kufanyika nchini imetokana na nchi hizo 54 kutambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na dawa za kulevya.

"Tanzania imepata nafasi kutokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya tano katika kupambana na dawa za kulevya hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Dawa za Kulevya na vitendo vya uhalifu (Unodc)," amefafanua Mwashusa.

Amesema kwamba katika mkutano huo wanatarajia jumla ya washiriki 120  watahudhuria ambapo miongoni mwao wamo washiriki wanaopambana kikamilifu na dawa za kulevya barani Afrika.

Mwashusa ameeleza sababu za kuuzungumzia mkutano huo ni kutaka kuufahamisha umma wa Watanzania kwani fursa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao kwa wageni.

Pia ni fursa ya kuutangaza utalii wa Tanzania na kufafanua kwa.kuwa kutakuwa na wageni wengi ni vema wakachangia fursa ya mkutano huo kufanya biashara.

Kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini amesema kwamba kwa sasa Tanzania wamefanikiwa kudhibiti na dawa za kulevya na kwamba Serikali imeweka mikakati ya kukomesha dawa za kulevya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.