Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Ashuhudia Mchezo Kati ya Namungo FC na Dodoma FC Mchezo Uliofanyiika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya mpira wa miguu  ya Namungo FC ya  Ruangwa na Dodoma FC baada ya mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kushuhudi mechi ya kirafiki kati ya Namungo FC ya Ruangwa na Dodoma FC, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu
 Rashidi Mpemba  (kushoto) wa Dodoma FC  na  Bruno John wa Namungo FC   wakiwania mpira katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu
 Rashidi Mpemba (kushoto) wa Dodoma FC akimiliki mpira huku akizongwa na  Bruno John wa Namungo FC  katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu
 Zahoro Pazi wa timu ya Dodoma FC  (kulia) akimtoka Luka Kikoti wa Namungo FC katika mchezo wa  kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu
 Zahoro Pazi  wa timu ya Dodoma FC  (kulia) na Luka Kikoti wa Namungo FC wakiwania mpira katika mchezo wa  kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Dodoma FC baada ya mechi ya kirafika kati ya timu hiyo na Namungo FC ya Ruangwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Namungo FC ya Ruangwa baada ya mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Dodoma FC iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.