Habari za Punde

Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Malide Nabii Zanzibar Wakuzungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanbzibar Balozi Seif Ofisini Kwake leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif  akizungumza na Kamati tendaji ya Jumuiya ya Milade Nabii Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kualikwa rasmi kushiriki Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad {SAW} yatakayotarajiwa kufanyika mnano Tarehe 19 Novemba 2018.
Sheikh Yussuf Abdulrahman akisoma dua mara baada ya kumalizika kwa kikao chao.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na. Othman Khamis OMPR.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Milade  Nabii Zanzibar Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.`
Katika mazungumzo yao Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sheikh Sheraly Shamsi alisema Maandalizi kwa ajili ya maadhimishio ya Maulidi ya Kitaifa ya uzawa wa Kiongozi wa Waumini wa Dini ya Kiislamu Ulimwenguni Mtume Muhammad {SAW} yamefikia hatua nzuri.
Sheikh Sheraly alisema Kamati Tendaji kupitia Wawakilishi wake katika maeneo mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba imeshafanya upembuzi na kuridhika na Madrasa zitakazoshiriki kwenye maulidi hayo yanayotarajiwa kufanyika mahali pake Uwanja wa Michezo wa Maisra Suleiman iwapo hakutakuwa na Mvua.
Alisema upembuzi huo umetoa fursa ya kupatikana kwa Madrasa kutoka kila wilaya ambapo zile za Kisiwa cha Pemba Wanafunzi wake wanatarajiwa kuingia Unguja mnamo Tarehe17 Novemba 2018 ambapo sherehe yenyewe itakuwa Jumatatu ya Tarehe 19 Vovemba 2018 sawa na Mwezi 11 Mfunguo Sita.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili waRais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Kamati Tendaji hiyo ya Jumuiya ya Milade Nabii kwa umakini wake unaopelekea kufanikisha maadhimisho ya Uzawa wa Mtume Muhammad {SAW} Kila Mwaka.
Balozi Seif  maulidi ya Mfunguo Sita yanaendelea kupata umaarufu hata nje ya mipaka ya Zanzibar kutokana na mikakati inayowekwa na Uongozi wa Kamati hiyo na kupelekea kuleta faraja sio kwa Waumini wanaohudhuria viwanjani hapo bali hata wale wanaofuatilia kupitia vyombo mbali mbali vya Habari wakiwa mitaani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.