Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Awapongeza Wananichezo wa Mahitaji Maalum Zanzibar Kwa Ushindi Walioupata Michuano ya Michezo ya Olimpic Yaliofanyika Zanzibara Mwaka Jana Uwanja wa Amaan.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mihayo Juma Nh’unga akimkaribisha Mgeni Rasmi Balozi Seif kuzungumza na Wanamichezo wenye Ulemavu walioshiriki mashindano ya Special Olympic.
Katibu Mkuu wa Special Olympic Tifti Musatafa Nahoda akielezea Historia ya Special Olympic kwenye hafla ya kuwapongeza Wanamichezo wenye ulemavu walioshiriki mashindano ya Special Olympic.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye Ucoclemavu Khalid Bakar Hamran akitoa Taarifakwenye hafla ya kuwapongeza Wanamichezo wenye ulemavu walioshiriki mashindano ya Special Olympic mwaka uliopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif akimpongeza Mwanamichezo Riziki Abdullah aliyepata tiketi ya kushiriki mashindano ya Madola ya Special Olympic yanayotarajiwa kufanyika Mwakani Nchini Abu Dhabi baada ya kushinda na kupata Medali ya Dhahabu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif akimpongeza na kumkabidhi medali ya Fedha Mwanamichezo Salama Kheir baada ya kushinda katika Mashindano ya Special Olympic mwaka uliopita.
Mchezaji Mtumwa Khamis akivishwa Medali ya Shaba na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuibuka kidedea kwenye mashindano ya Special Olympic.
Baadhi ya Wanamichezo  Wenye Ulemavu walishiriki mashindano ya Special Olympic mwaka uliopita na kufanikiwa kujinyakulia Medali 38 wakiwa katika tafija maalum ya kupongezwa hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil.
Balozi Seif  kati kati ya waliokaa kwenye viti akiwa katika picha ya pamoja na Wanamichezo wenye ulemavu walioshiriki mashindano ya Special Olympic na kuibuka na Medali 38 za Dhahabu, Shaba na Fedha.

 Balozi Seif akiagana na baadhi ya Viongozi wa Taasisi zinazo jishughulisha na Watu wenye ulemavu Nchini mara baada ya kuhudhuria hafla ya kuwapongeza wanamichezo walemavu waliofanya vyema kwenye mashindano yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.