Habari za Punde

Wanamichezo Wenye Mahitaji Maalum Wapongeza Kwa Ushindi Wao Katika Michuano ya Watu Wenye Ulemavu Specily Olympic Yaliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza na kumkabidhi medali ya Fedha Mwanamichezo,Mwanafunzi Salama Kheir baada ya kushinda katika Mashindano ya Special Olympic yaliofanyika mwaka jana hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba ushirikishwaji wa Watu wenye ulemavu kwenye  Michezo mbali mbali ndio njia muwafaka inayoweza kuwasaidia kuleta marekebisho ya tabia na mienendo mizuri kwa kundi hilo la Mahitaji Maalum kutokana na kuwa Michezo ni kinga na afya.
Alisema kundi la Watu wenye Mahitaji Maalum wana uwezo na vipaji vya kufanya mambo makubwa endapo watapatiwa fursa za kutosha za kutumia vipaji vyao, ujuzi na uwezo waliotunukiwa na Mwenyezi Muungu.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo kwenye tafrija ya kuwapongeza Wanamichezo wenye Ulemavu wa Akili  hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni ambao walishiriki Mashindano ya Michezo ya Watu wenye Ulemavu    {Specily Olympic} iliyofanyika mwishoni mwa Mwaka uliopita kwenye Uwanja wa Aman.
Alieleza kwamba ni jambo zuri lililofanywa na Idara ya Watu wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Jumuiya na Taaisi nyengine kuona ipo haja ya kuwakutanisha Wanamichezo wenye Ulemavu wa Akili na kuwapongea kwa aina ya kipekee.
“ Watu wenye Ulemavu tukiwashirikisha kwenye Michezo mbali mbali itaweza kusaidia kuleta marekebisho ya tabia na mienendo  mizuri ya Watu haokutokana na kuwa Michezo ni Kinga na Afya”. Alifahamisha Balozi Seif.
Alisema zipo changamoto mbali mbali zinazowakabili Watu wenye Ulemavu wa Akili ikiwemo kunyanyapaliwa kutoka kwa baadhi ya Watu na hatimae inapeleka kukoseshwa haki zao za kupata Elimu, Afya, Ajira, mchanganyiko ndani ya Jamii sambamba na ushiriki wa Michezo tofauti.
Balozi Seif  alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kupambana na mitazamo hasi kwa kuendelea kuwaelimisha Wananchi pamoja na kujenga mazingira mazuri zaidi, kupitia sheria, Sera na Miongozo kwa Watu wenye Ulemavu wa Akili ili kupatab haki zao kama Watu wengine.
Aliwanasihi Wananchi kuwa umefika wakati wa kubadili misimamo na mitazamo juu ya wanavyowaona na kuwachukuliwa Watu wenye Ulemavu wa Akili kuwa ni mzigo katika Familia na Jamii kwa ujumla.
Balozi Seif aliweka wazi kwamba Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa itahakikisha Mikakati na Mipango iliyoweka katika kuimarisha mazingira mazuri kwa Watu wenye mahitajio maalum inaendelea kutekelezwa vyema ili kupata Ustawi mzuri  na wa pamoja kwa Makundi yote ya Kijamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewapongeza Wazazi, Walezi na Wanamichezo wenye Ulemavu kwa michango na mashirikiano ya karibu yaliyosaidia kufanikisha mashindano ya Michezo  ya Watu wenye Ulemavu wa Akili ambao Vijana wa Zanzibar walipata fursa ya kuvitangaza vipaji walivyonavyo.
Alisema shukra za kipekee ziende kwa waandaaji wa Mashindano hayo kwa anaelewa kwamba wamepata vikwazo vingi katika kuandaa na kusimamia michezo hiyo na kuwaomba wasivunjike moyo kwa vile vikwazo ni ni sehemu ya kufanikisha Maendeleo yoyote yale.
Balozi Seif aliwaomba Vijana hao wa Zanzibar waviendeleze vipaji hivyo vilivyoibua Medali 38 kati ya hizo 19 dhahabu, 9 shaba na 10 fedha ili kujenga Heshima kwao pamoja na Taifa lao kwa ujumla.
Akitoa Taarifa  Katibu wa Special Olympic Zanzibar Tifli Mustafa Nahoda  alisema Special Olympic ni mpango Maalum uliobuniwa kutoa nafasi ya kujitathmini kwa Watu wenye Mahitaji Muhimu namna wanavyoshirikisha katika masuala ya Kijamii.
Mustafa alisema Mpango huu uliasisiwa Nchini Marekani Mnamo Mwaka 1968  kwa kujumisha Nchi Wanachama 180 ukishirikisha Wanamichezo wapato Milioni Mbili.
Alisema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha  Special Olympic Mwaka 1986 ikiishirikisha Zanzibar ambayo kwa upande wake ikaanisha ile ya Zanzibar Mwaka 2007 na kusajiliwa Baraza lka Michezo Zanzibar.
Alifahamisha kwamba uanzishwaji wa Mpango huo umeiwezesha Zanzibar kupiga hatua kubwa ya kujitangaza Kitaifa na Kimataifa kutokana na kuibuka na Medali nyingi wakati wanamichezo wake wanaposhiriki katika Mashindano mbali mbali.
Mustafa alieleza kwamba ushindi wa wachezaji wa Zanzibar wenye Mahitaji Maalum umefanikisha ujenzi wa Imani kwa Wanajamii jinsi Vijana wenye uklemavu walivyoshiriki vyema na hatimae kuonyesha uwezo wao wa kiajabu.
Hata Hivyo Katibu Mkuu huyo wa Special Olympic Zanzibar alisema zipo changamoto zinazochangia kukwaza maendeleo ya Kundi hilo akizitaja baadhi kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa Maalum vya wanamichezo wenye Ulemavu pamoja na ukosefu wa Ofisi wanaolazimika kuhamia kila sehemu.
Kwa upande wake Kaimu Kurugenzi wa Idara y Watu wenye Ulemavu Zanzibar Khalid Bakar Hamran alisema kuanzishwa kwa Michezo ya Watu wenye Ulemavu Nchini kumelenga kuwajengea uwezo Watu wenye Kundi Maalum ili washiriki kikamilifu katika harakati zote za Kijamii.
Khalid alisema juhudi hizo zimeiwezesha Zanzibar kushiriki na kushinda mashindano yote yanayoandaliwa na kuwashirikisha Watu wenye mahitaji Maalum.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Abdullah Hassan Mitawi kwa niaba ya Kundi la Watu wenye ulemavu amemshukuru na kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ukaribu wake wa kuwa na Watu wenye mahitaji Maalum wakati wote.
Abdullah Mitawi alisema mjumuiko wake huo unaendelea kuithibitishia Jamii kwamba amekubali kujitolea kwa moyo wake uliojaa busara na hekima kuliunga mkono Kundi hilo hasa katika kulipigania na changamoto inazolikumba ikiwemo masuala ya udhalilishaji.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika Hafla hiyo Naibu Waziri Wilaya ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mihayo Juma Nh’unga  alivikumbusha Vyombo vya Dola Nchini kuendelea kutekeleza jukumu lao ikiwemo kuwachukulia hatua za kuwafichua Watu wenye tabia ya kuwafisha Watu wenye matatizo ya akili.
Naibu Waziri Nh’unga  alisema kundi la Watu wenye mahitaji Maalum lina haki kamili ya kupata fursa na nafasi kama wanavyopata watu wengine kwani bado wapo watu wanaohisi kwamba wale wenye ulemavu hawapaswi kushiriki michezo kutokana na hali zao.
Aliwapongeza Walimu, Wakufunzi na wasimamizi waliowezesha Vijana wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla walowezesha kupatikana Vijana Wawili wa Tanzania kupata vigezo na sifa za kushiriki michezo ya Madola ya Olympic inayotarajiwa kufanyika Nchini Abu Dhabi Mwaka 2019.
Balozi Seif  katika hafla hiyo alikabidhi Medani hizo  kwa Wachezaji 38 walioshinda Mashindano hayo  ambao kati ya hao washindi 19  ni dhahabu, 9 shaba na 10 fedha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.