Habari za Punde

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume Mgeni Rasmin. Katika Tamasha la Urithi Wetu.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Balozi Ali Abeid Karume  akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa kikundi cha Baba Watoto Bwana. Mgunga Mwamnyenyelwa mara baada ya kikundi hicho kumaliza onesho lake jukwaani kwenye tamasha la Urithi Wetu, mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.


Na Andrew Chale, Dar
Kundi la Babawatoto Centre linalofanya sanaa mbalimbali hapa nchini mwishoni mwa wiki limetia fora kwa kutoa burudani safi na ya kipekee kwa watu mbalimbali waliofika kwenye tamasha la Urithi Wetu (Urithi Festival) Jijini Dar es Salaam.
Kundi hilo  limeweza kufanya onyesho ambalo lilikuwa na mchanganyiko wa sarakasi ya maigizo lililohamasisha na kusisistiza umuhimu wa vijana kufuata utamaduni  wa asili ambapo.
Kikundi hicho kinachoundwa na vijana wanaoishi katika mazingira magumu, kilikonga nyoyo za mamia ya watazamaji waliofika kwenye kilele cha ufungaji wa Tamasha hilo kwa Mko wa wa Dar es Salaam kutokana na umahiri wao wa kulishambulia jukwaa hasa katika fani ya sarakasi mara zote wananchi waliinuka vitini kwa shangwe.
Vijana hao kwa siku mbili walizopata nafasi kwenye tamasha hilo wamejikusanyia mashabiki kutokana na uwezo wao mkubwa katika fani ya sarakasi ambapo wameonyesha umahiri na kumudu vyema michezo ya miruko, trapeze na ngoma za asili.
Baba Watoto ni kundi  lililo chini ya Shirika lisilo la Kiserikali lenye makao makuu yake Mburahati kwa Jongo, jijini Dar es Salaam chini ya Bwana Mgunga Mwamnyenyelwa.
Mbali na Babawatoto Centre, pia vikundi na wasanii mbalimbali walipata kufanya maonesho yao ambapo kwa mwaka huu tamasha hilo la Urithi ni la kwanza likiandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuongeza vivutio vya wageni kuendelea kufurahia Urithi wa Mtanzania awapo hapa nchini.
Tukio hilo limfanyika katika viwanja vya Kijiji cha Makumbusho huku mgeni rasmi aliyefunga tamasha hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Balozi Ali Abeid Karume  aliwahimiza watanzania kuendelea kuulinda utamaduni wa Mtanzania kwa misingi yake kwa kurithi yale yoet mazuri.
Wasanii wa Kikundi cha Sarakasi wakionesha umahiri wa mchezo huo wakati wa Tamasha la Urithi Wetu Tanzania 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.