Habari za Punde

Jumla ya Wananchi 1,452 Wamejitokeza Kupima Afya Zao. Katika Kambi ya Madaktari Mabingwa Kutoka Saud Arabia na Misri.


Na. Shaib Kifaya - Pemba.
Jumla ya Wagonjwa wapatao 1,452,  wamefanyiwa uchunguzi  wa maradhi mbali mbali na wagonjwa 321 kati ya hao wamefanyiwa upasuaji  wa maradhi tofauti kwa Hospitali za Wete na Chake Chake katika kambi ya madaktari bingwa kutoka nchini Saudia Arabia na Misri wakiwa ni wafanyakazi wa  Jumuiya ya Kiislamu WAMY.

Kambi hiyo ya madaktar i iliyofika Kisiwani Pemba, kwa ajili ya kutowa huduma hizo bure  ilizinduliwa rasmi tarehe 13/10/2018 na  Waziri wa afya Zanzibar, Hamadi Rashid Muhammed ,huko hospitali ya Chake Chake na kumalizika tarehe 24/10 mwaka huu.

 Akitoa maelezo kwa wagonjwa waliofanyiwa  upasuaji  Daktari dhamana wa hospitali ya Chake Chake, Dk, Khatibu Shaame Khatibu ,alisema wananchi walijitokeza kwa wingi na kuweza kupatiwa uchunguzi na kutibiwa kwa kadri ya maradhi yaliokuwa yakiwasumbuwa.

Alisema magonjwa ya akina mama waliofanyiwa upasuaji ni 25 ,maradhi mbali mbali kwa watoto 86,kama vile Ngiri maji,Mdomo Sungura mdomo upande, na apendex, kwa  watu wazima  , 46 upasuaji magonjwa mbali mbali yakiwemo Goita, Ngiri maji,na waliofaniyiwa upasuaji wa mifupa ni 5 na Mkojo ni 3 .

Dk, Khatibu, alisema kwamba madaktari hao waliwapa mashirikiano ya kutosha kwenye kazi yao kwa vile  walikuwa na madktari pamoja na wazalendo wa ndani ambao wameweza kupata kujifunza zaidi.

“Kwa kweli tunawashukuru timu ya madaktari hawa  kutoka Falme za Kiarabu kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika huduma za kusaidia kutoa matibabu ‘’,alisema .

Kwa upande wake Msaidizi Muuguzi kutoka Hospitali ya Wete,  Dk, Sabra Salum  Seif, alisema wananchi walijitokeza kwa wingi katika hospitali kwa ajili ya kutibiwa na kufanyiwa uchunguzi ambapo  walipatiwa matibabu bila ya usumbufu.

Alieleza kwa wagonjwa waliofanyiwa uchunguzi ni  25 na uperesheni  kwa mangonjwa ya maradhi mbali mbali ni  84 ambao ni watu wazima  na Magonjwa ya viungo bandia 24 , Mifupa 24 magonjwa ya akina mama ni 25
.
Nae, Afisa Tiba kutoka Wizara ya afya Pemba, Dk Yussouf Hamad Idi, alisema kwamba timu ya madaktari hao imewasaidia wananchi wengi Kisiwani humo kwani  wengi wao hawana uwezo wa kujitibu na kubakia kuathirika na maradhi  bila ya kupatiwa tiba.

Aidha aliwaomba wananchi kuthamini juhudi za Serikali iliyopo madarakani kwani imekuwa ikihudumia wananchi wake na kuboresha huduma zilizo bora.

Nae Dk, Ramadhan Faki Ali , anae husika na mambo ya Upasuaji , alisema kesi nyingi ni mishipa ya hania ama ngiri inayosabibishwa na kufanya kazi za nguvu kwa watu hao.

Amina Omar Salum,  mkaazi wa Madungu Chake Chake, ambaye ni miongoni mwa wagonjwa waliofanyiwa upasuwaji hospitali ya Chake,  aliwashukuru madaktari hao kwa kufika Kisiwani Pemba na kuweza kuwatibubila malipo.

‘’Kwa kweli namshukuru Mungu sihaba hali yangu inaenda vizuri baada ya kufanyiwa upasuwaji kwa  matatizo  nilio kuwa nayo sasa limeniondokea’’,alisema.

Kwa upande wake,  Ofisa Mdhamini Wizara ya afya Pemba, Shadya Shaaban Seif, aliwashukuru madaktarI hao kwa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kuamua kujitolea kutoa matibabu bure kwa wananchi wa Kisiwa cha Pemba.

Hata hivyo aliwataka madaktari hao kuzidi kuwaunga mkono wananchi wa Zanzibar na Serikali yao  kwa kuwasaidia kwenye shughuli za kimaendeleo na kuwaahidi uhusiano huo utaendelezwa ambao ulianzishwa na Viongozi wakuu wa nchi waliotangulia mbele ya haki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.