Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Azungumza na Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Ulinzi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma akizungumza na Wakuu  wa Wilaya pamoja na Wakuu wa Ulinzi na Usalama kuhusiana na maandalizi ya kuanza kwa mtihani wa darasa la nne,sita,kidatu cha pili pamoja na kidatu cha nne huko katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Vuga
Mkuu  wa Mkoa Mjini Magharibi Ayuob Mohamed Mahamuod akizungumza na wakuu  wa Wilaya  pamoja na Wakuu wa ulinzi na Usalama kuhusiana na maandalizi ya kuanza kwa mtihani wa darasa la nne,sita, Kidatu cha pili pamoja na kidatu cha nne (Picha na Kijakazi Abdalla Habari Maelezo) 
Na Mwashungi Tahir.  Maelezo Zanzibar.   31-10-2018.                                                                      WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma aliwataka   walimu                   wanaosimamia mitihani wawe waangalifu  katika usimamizi na kuepuka  na mambo yasiyofaa kwenye vyumba vya mitihani na kwa wananfunzi wanaofanya mitihani.
Hayo amesema huko ofisini  kwa Mkuu wa Mkoa Vuga wakati alipokuwa akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa Wilaya  na Mikoa , Wakurugenziwa Wizara ya Elimu na waandishi wa habari kwenye kikao cha kuzungumzia kujiandaa na mitihani ya kidato cha nne darasa la sita na darasa la kumi na darasa la nne.
Alisema mitihani inaletwa  na ina  ulinzi mkubwa na usalama wa kutosha , na kuitaka kamati ya ulinzi na usalama iwe makini kuhakikisha mitihani yote inafanywa kwa usalama  na kutarajia mitihani hiyo  inafanyika kwa amani bila ya udanganyifu wowote .
Aidha akitoa tahadhari kwa walimu wanaosimamia  mitihani waache udanganyifu  na kuwataka wawe makini katika usimamizi wao  wakibainika wamehusika na udanganyifu huo vyombo vya ulinzi na usalama itawachukulia hatua  kwani tegemeo letu Zanzibar ifanye vizuri .
“Natoa tahadhari kwa walimu wanaosimamia mitihani mujiepushe na suala zima la udanganyifu  mwalimu akibainika kajihusisha vyombo vya ulinzi vitafanya kazi yake na Wizara pia”.Alisema Waziri huyo.
Alisema tunatarajia wanafunzi wazuri  wafaulu mitihani  yao kwa akili zao ili waweze kuendelea hadi kidatu cha sita  na kuingia kwenye chuo ili baadae tuje kupata wazalendo wazuri katika majukumu ya Serikali hapo baadae kwani wao ndio tegemeo la baadae .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  ambae pia Kaimu wa Mkoa wa Kusini  Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka walimu wawasimamie wanafunzi katika mitihani yao vizuri na kujiepusha na udanganyifu kwani anatarajia matokeo mazuri katika Mkoa wake .
Akitoa wito kwa walimu aliwataka wasimruhusu mwanafunzi kufanya mitihani ikiwa hana sifa na akitokea mwalimu akimruhusu mwanafunzi kufanya mitihani basi sheria haitomuwachia zitamuondosha yeye.
“Iwapo mwalimu atamruhusu mwanafunzi kufanya mtihani akiwa hana sifa zinazostahiki kufanya mtihani basi mwalimu huyo ahakikishe atajiharibia sifa yeye”.Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Pia alisema kila Mwalimu Mkuu na wasimamizi wa mitihani wawe waangalifu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi na kuona wanafunzi wanafanya mitihani yao kwa usalama na utulivu.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya mtihani Mkoa wa Mjini  Hamida Mussa Khamis  alisema kamati iliweza kusimamia utaratibu wa mitihani na imekwenda vizuri kama ilivyopangwa.
Alihakikisha ulinzi ulikwenda vizuri wala hakutokuwa na changamoto zozote na wala suala la udanganyifu hautotokea na tunaahidi  mitihani itafanyika vizuri bila mivujo wala udanganyifu wowote na kuwataka wanafunzi wawe watulivu katika kufanya mitihani yao.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.