Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akibadilishana mawazo na Timu ya Uongozi wa juu wa Benki ya Dunia {World Bank} ukiongozwa na Mratibu wa Benki hiyo Bwana Muderist Abdillah baada ya kutembelea baadhio ya miradi ya Tasaf Visiwani Zanzibar.Kulia ya Balozi Seif ni Mratibu wa Benki hiyo Bwana Muderist Abdillah na Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzannia {Tasaf} Nd. Ladislaus Mwamanga.
Uongozi wa juu wa Benki ya Dunia {World Bank} ukiongozwa na Mratibu wa Benki hiyo Bwana Muderist Abdillah ulikutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf} chini ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif akiagana na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Dunia baada ya mazungumzo yao walipofika Zanzibar kufanya ziara ya siku moja kukagua Miradi ya Wananchi inayosimamiwa na Mfuko wa Tasaf.
Balozi Seif akiagana na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Dunia baada ya mazungumzo yao walipofika Zanzibar kufanya ziara ya siku moja kukagua Miradi ya Wananchi inayosimamiwa na Mfuko wa Tasaf.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif,kati kati waliokaa Vitini akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Uongozi wa Benki ya Dunia pamoja na ule wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bara na Zanzibar baada ya Timu hiyo kutembelea baadhi ya Miradi ya Wananchi inayosimamiwa na Mfujko wa Tasaf.
Balozi Seif akiagana na baadhi ya Viongozi wa Benki ya Dunia baada ya mazungumzo yao walipofika Zanzibar kufanya ziara ya siku moja kukagua Miradi ya Wananchi inayosimamiwa na Mfuko wa Tasaf.
Picha na – OMPR – ZNZ.


Na.Othman Khamis OMPR.
Benki ya Dunia imeithibitishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Fedha itaendelea kuongeza nguvu zake za uwezeshaji na Taaluma katika kuona miradi ya Maendeleo iliyoanzishwa na Wananchi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf} inafanikiwa katika utekelezaji wake.                                                                 

Mratibu wa Benki ya Dunia {World Bank} Bwana Muderist Abdillah aliyeiongoza Timu ya Viongozi wa Taasisi hiyo ya Fedha iliyofanya ziara ya siku Moja Visiwani Zanzibar kuangalia maendeleo ya Miradi iliyo chini ya Mfuko wa Tasaf alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
                                                                                                  Bwana Abdillah alisema Uongozi wa juu wa Benki ya Dunia {World Bank} umefurahishwa na jitihada kubwa zinazochukuliwa na Wananchi walio wengi Visiwani Zanzibar katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Jamii inayosimamiwa na Tasaf.
Alisema Kizazi Kipya kinachoshuhudia jitihada hizo za Wazazi wao katika kuwajengea misingi na Miundombinu Bora ya Kimaisha kitafaidika na Miradi hiyo iliyolenga zaidi katika Sekta za Ustawi wa Jamii ikiwemo Afya, Elimu pamoja na Kilimo.
“ Umakini wa Wananchi katika utekelezaji wa miradi ya Tasaf  umeleta faraja kubwa kwa Benki ya Dunia ambayo ndio mdau mkubwa wa uwezeshaji wa Miradi hiyo ”. Alisema Bwana Abdillah.
Mratibu huyo wa Benki ya Dunia alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Taasisi hiyo ya Kifedha ya Kimataifa itaendelea kuunga mkono muda wote miradi ya Wananchi wenye Kipato cha Chini.

Aliupongez na kuushukuru Uongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Taasisi zilizopewa jukumu la kusimamia Miradi ya Tasaf kwa umahiri na usimamizi wao mkubwa unaoendelea kuleta mafanikio makubwa.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf } Nd. Ladislaus Mwamanga amesema kazi kubwa inayofanywa na Wananchi wa Zanzibar kwenye miradi ya Maendeleo kupitia programu zinazosimamiwa na Mfuko huo imeleta mafanikio makubwa.
 Alisema Zanzibar imeweza kuweka rekodi nzuri katika utekelezaji wa Miradi yote inayosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf} katika Awamu zote na kuipelekea Tanzania kupanda hadhi Duniani kwenye Miradi inayopata Ufadhili wa Kimataifa.
Mwamanga amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko huo itaendelea kuongeza nguvu katika kuona kundi kubwa la Wananchi walio na kipato duni hasa Vijijini wanaongezewa nguvu za uwezeshaji ili kuondokana na mazingira magumu yanayowakabili.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini Tanzania {Tasaf} unaopata msukumo kupitia Benki ya Dunia umeleta Ukombozi Mkubwa hasa kwa Wananchi wa Kisiwa cha Pemba.

Balozi Seif alisema kundi kubwa la Wananchi wenye mazingira magumu ambao wameorodheshwa kwenye Mpango Maalum wa Kaya Maskini katika Shehia mbali mbali Unguja na Pemba limefanikiwa kupunguza kwa kiasi Fulani ukali wa Maisha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiahidi Benki ya Dunia kupitia Ujumbe wake huo wa Viongozi kwamba Serikali zote mbili Nchini Tanzania zitaendelea kusimamia Miradi hiyo ili iwe ya kudumu na kuleta Ustawi kwa Jamii yote Nchini.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.