Habari za Punde

Meli ya Kurikodi Mtetemo ya Kina Kifupi Cha Maji Yawasili Zanzibar Kwa Ajili ya Utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.

Meli kubwa itakayotumika kurekodi taarifa za mtetemo kwa kina kifupi cha maji wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Unguja na Pemba ya Stanford Bateleur ikiwa imefunga gati Bandari Malindi ikiwa tayari kuanza kazi hiyo wiki ijayo.
Nahodha wa meli ya Stanford Bateleur Raul Mendoza akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu meli hiyo inavyofanyakazi ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji 
Mkurugenzi Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa utafutaji na Uchimabaji wa Mafuta na Gesi AsiliaOmar Zubeir Ismail akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa meli ya Stanford Bateleur inayorekodi mtetemo katika kina kifupi cha maji.

(Picha na Ramadhan Ali -Maelezo Zanzibar)

Na  Mwashungi Tahir.  Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji Mamlaka ya Udhibi wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Omar Zubeir Ismail  alisema SeriKali ya Mapinduzi ya Zanzibar  inaendelea na utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya mtetemo kwa kitalu cha Pemba Zanzibar.
Hayo ameyasema leo huko Bandarini Malindi wakati alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasili meli kubwa ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kina kifupi cha maji.

Aidha alichukua nafasi kwa kuwajuilisha wananchi  kazi ya utafiti wa mafuta na gesi Asilia kwa njia ya mtetemo bado inaendelea kwa upande wa kina kifupi cha maji (TRANSITION ZONE 2D SEISMIC SURVEY) katika maeneo ya visiwa hivyo.
“Nachukua nafasi hii kuwajuilisha wananchi  kwamba suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ni la muda mrefu na linaweza kufika hadi miaka kumi kukamilika nawaomba muendelee na kazi zenu za kawaida”. Alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema tumuombe Mungu tufanikiwe suala hili kwani likifanikiwa ni la wote kwa maendeleo ya nchi yetu na vizazi vyetu vya hapo baadae.
Pia alisema meli zitakazotumika katika zoezi la mtetemo kwa kina kifupi cha maji tayari zimeshawasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.
Mkurugenzi huyo alielzea meli zitakazotumika ni MV DP STANFORD  yenye urefu wa mita 86 ambayo itatumika kwa ajili ya kurikodi taarifa za mtetemo.nyengine ni MV HAIBAO yenye urefu wa mita 25 ambayo tatumika kwa ajili ya kutoa mawimbi sauti na kutakuwa na CHASE BOAT NA FAST BOAT ambazo zitatumika kwa ajili ya kutoa ulinzi wakati wa zoezi hilo pamoja na boti ndogo ndogo zinazoitwa RUBER BOAT kwa ajili ya kubebea vifaa.
Alisema zozi hili liko chini ya dhamana ya kampuni ya RAKGAS ya nchini RAS-AL KHAIMAN na linafanywa na Kampuni ya BGP INTERNATIONAL yenye makao Makuu  yake nchini China na zoezi hilo linasimamiwa na taasisi za Serikali ambazo ni mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar (ZPRA) na kampuni ya maendeleo ya mafuta na gesi asilia ya Zanzibar (ZPDC).
Vile vile alisema tarehe 27-Oktoba 2017 ilizinduliwa  Meli utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa kutumia meli maalum ya Kampuni ya BGP kutoka China kwa ajili ya kufanya zoezi la mtetemo katika kina kirefu cha maji baharini na  kazi hiyo ilikamilika mnamo tarehe 28 Novemba 2017 katika visiwa vya Pemba na U nguja na kazi hiyo ya mtetemo kwa maeneo ya ardhini nchi kavu  kwa visiwa hivi imeshakamilika.

Nae Nahodha wa MV Stanford Bteleur Raul Mendoza alisema kazi ya utafitaji wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji itachukua kiasi ya miezi miwili kukamilika kwa Unguja na Pemba.

Picha No. 01 -Meli kubwa itakayotumika kurekodi taarifa za mtetemo kwa kina kifupi cha maji wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Unguja na Pemba ya Stanford Bateleur ikiwa imefunga gati Bandari Malindi ikiwa tayari kuanza kazi hiyo wiki ijayo.

Picha No. 02 - Nahodha wa meli ya Stanford Bateleur Raul Mendoza akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu meli hiyo inavyofanyakazi ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji 

Picha No. 03 - Mkurugenzi Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa utafutaji na Uchimabaji wa Mafuta na Gesi AsiliaOmar Zubeir Ismail akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa meli ya Stanford Bateleur inayorekodi mtetemo katika kina kifupi cha maji.

PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.