Habari za Punde

Mufti Mkuu wa Tanzania Azindua Maandalizi ya Ijitimai ya Kimataifa Itakayofanyika Zanzibar.

Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi Khamis wa kwanza (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Alhaji Mwalim Hafidhi Jabu kukagua Mskiti unaotarajiwa kufanyika Ijitimai ya kimataifa huko Kidoti.
Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi Khamis akimkaribisha Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali katika uzinduzi wa maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa itayofanyika tarehe 22/02/2019 huko kijiji cha Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akizindua rasmin maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa itayofanyika tarehe 22/02/2019 katika Kijiji cha Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja uzinduzi huo umefanyia Msikiti wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Kidoti.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akimsalimia Bii. Mwajuma juma mkaziwa Kidoti alietoa kiwanja kwa ajili ya kujengwa Mskiti huo.
Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.