Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari, (Sustainable Blue Economy Conference ) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli.
Na.Suzan Kunambi.Nairobi Kenya.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,amesema
Tanzania imejidhatiti katika kutoa ushirikiano unaohitajka katika utungaji wa
sera na sheria mbali mbali zinazohusu sekta ya
uchumi wa bahari pamoja na kushiriki katika kutafuta nyenzo na
rasilimali muhimu katika utekelezaji wa mipango iliyopangwa katika sekta hiyo.
Dk. Shein aliyasema
hayo leo katika ufunguaji mkutano wa
uchumi endelevu wa bahari kwenye ukumbi wa Kenyatta Mjini Nairobi,wakati akitoa tamko
la Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu mipango ya hivi sasa na
baadae katika kuendeleza nyanja uchumi
wa bahari.
Alisema kuwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inategemea sana rasilimali bahari, mito na
maziwa katika shughuli muhimu za kiuchumi na kijamii . Alieleza kwamba
rasilimali hizo zinaiunganisha Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na mataifa mengine duniani katika sekta ya
usafiri na mawasiliano, sambamba na kutumika katika kuimarisha biashara, utafutaji wa madini, uendelezaji wa sekta ya nishati, kukuza
uvuvi, utalii na shughuli nyengine za
kiuchumi na kijamii.
Alifahamisha
kwamba kutokana na umuhimu wa rasilimali
hizo katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na utekelezaji wa mikakati ya kupunguza
umasikini, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kupanga na kutekeleza mipango yenye lengo la
kuziimarisha na kuzilinda rasilimali
hizo dhidi ya changamoto na athari mbali mbali; zikiwemo
zinazosababishwa na shughuli za binaadamu.
Dk.Shein alizibainisha baadhi ya
athari na changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira, ukame, kuongezeka kwa
kina cha maji ya bahiri na majanga mbali mbali yanayaosababishwa na mabadiliko
ya tabia nchi.
Alihimiza haja ya
mataifa duniani pamoja na taasisi za kitaifa na kimataifa kuungana
pamoja kwa ajili kupanga na kutekeleza mikakati madhubuti zaidi itakayowezesha kuondoa changamoto hizo.
Alieleza kwamba juhudi za pamoja zinahitajika hivi sasa, katika utekelezaji wa mipango na ajenda za kuimarisha uchumi wa
bahari katika ngazi za kitaifa na kimatafifa
kwa kuzingatia mipango iliyopo hivi
sasa na inayoendelea kupangwa.
Vile vile,
asisitiza kwamba ili kupata mafanikio ya kweli katika katika kupanga na
kuteleza mipango ya uchumi wa bahari na lazima sekta binafsi na jamii kwa jumla
zishirikishwe kikamilifu.
Alimalizia kutoa
tamko hili kwa kuelezea imani yake
kwamba maazimio yatakayopitishwa katika
mkutano huo, yakakuwa na mchango mkubwa
katika kuendeleza uchumi wa bahari na
kutoa mwelekeo mpya katika kuyafikia
malengo Endelevu ya dunia na kuimarisha
ustawi wa watu wote duniani.
Aidha Dk. Shein alitoa shukurani na
pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Kenya
pamoja na Serikali ya Canada na Japan kwa kuandaa mkutano huu maalum wa Uchumi Endelevu wa Bahari.
Mapema akifungua mkutano huo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwashukuru
wajumbe kutoka pande mbali mbali za Dunia kwa kushiriki kwa wingi katika
mkutano huo uliolenga kuweka mikakakati itakayosaidia kutumia bahari,mito na maziwa
kwa kukuza uchumi wa nchi na rasilimali hizo.
Akitoa tamko la Serikali yake Rais Kenyatta alielezea dhamira na
muelekeo wa
Serikali hiyo katika kuendeleza na kuzisimamia uchumi wa bahari na
kusema kuwa Kenya itashirikiana na nchi mbali mbali na jumuiya za kimataifa
katika kuendeleza uchumi huo wa bahari.
Mkutano huo wa siku tatu
uliondaliwa na Serikali ya Kenya kwa kushirikiana na Canada na Japan umeshirikisha
nchi 180 na washiriki zaidi ya 13,000 kutoka taasisi mbali za binapsi,za kiserikali,wajasiriamali
na makundi ya vijana na wanawake na watu wenye ulemavu.
No comments:
Post a Comment