Habari za Punde

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Yapokea Karatasi za Kupigia Kura Uchaguzi Mkuu 2025

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Thabit Idarous Faina (kushoto) akisaini hati za makabidhiano ya Karatasi za Kupigia Kura na Mkurugenzi  Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar Ndg.Frank Kagoma (kulia) hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
Mkurugenzi wa ZEC, Thabit Idarous Faina (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar, Frank Kagoma wakikabidhiana nyaraka baada ya kupokea karatasi za kupigia kura makao makuu ya ZEC Unguja Zanzibar
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Thabit Idarous Faina akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakati wa kupokea karatasi za kupigia kura, hafla hiyo iliyofanyika kati Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Maisara Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.  
Baadhi ya Waangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar  wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg.Thabit Idarous Faina akizungumza wakati wa hafla ya kupokea karatasi za kupigia kura.  
Mwenyekiti wa (ZEC) Mhe.Jaji Goerge Joseph Kazi  na Makamu Mwenyekiti wa (ZEC) Mhe.Jaji Aziza Iddi Suwedi wakiwa na Wajumbe wa (ZEC) wakifuatilia hafla ya mapokezi ya karatasi za kupigia kura Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar  2025, hafla hiyo iliyofanyika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara Wilaya Jijini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg,Thabit Idarous Faina akionesha mfano wa Karatasi ya kupigia kura kwa waandishi wa habari wakati wa mapokezi ya karatasi hizo uliyofanyika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.


Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2025 wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg.Thabit Idarous Faina akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katibu wa Kamati ya Maalum ya NEC,Idara ya Organizesheni CCM Zanzibar Ndg.Omar Ibrahim Kilupi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya mapokezi ya Karatasi za kupigia Kura Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar oktoba 2025 , kutowa shukrani kwa Tume kwa maandalizi mazuri kuelekea uchaguzi. 
Mwanasheria Mkuu wa ACT-Wazalendo Mhe.Omar Said Shaban akizungumza wakati wa hafla ya mapokezi ya karatasi za kupigia kura uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Oktoba 2025, kuipongeza Tume ya Uchaguzi kwa maandalizi mazuri kuelekea uchaguzi oktoba 2025.
Mwakilishi wa Chama Cha ADA -TADEA  Ndg. Ali Mohammed Ali  amesema wameridhishwa hatua hiyo ya maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kwa kushirikishwa Wadau wa Uchaguzi kila hatua jambo ambalo linaondoa sitofahamu zinazoweza kujitokeza. 
MUANGALIZI wa  ndani wa Uchaguzi Mkuu kutoka Jumuiya ya JUMAMU Bi.Salam Shaban Khamis akizungumza na wakati wa hafla ya mapokezi ya karatasi za kupigia kura Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Oktoba 2025.hafla hyo iliyofanyika Afisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara Wilaya ya Mjini Ugunja Jijini Zanzibar leo 18-10-2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.