Habari za Punde

Wazanzibar Wanaoishi Nchini Canadia Diaspora wa Jumuiya ya ZACADIA Wakabidhi Vifaa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar.

Baadhi ya Wheel Chair zilizotolewa na Wazanzibar Wanaoishi Nchini Canada, kwa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Zanzibar Ndg. Hassan Khatib Hassan, akimkabidhi Wheel Chair Mkurugenzi wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar B. Abeda Rashid Abdallah,msaada huo umetolewa na Wazanzibar wanaoishi Nchini Canada Diaspora ZACADIA, kushoto Meneja wa ZACADIA Bi. Firdaus Rashid Tabia, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Idara ya Watu Wenye Ulemavu Migombani Zanzibar.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Zanzibar Ndg. Hassan Khatib Hassan, akizungumza wakati wavkukabidhi msaada wa wheel chair, zilizotolewa na Wazanzibara Diaspora Wanaoishi Nchini Canada wa Jumuiya ya ZACADIA, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya Ofisi za Idara ya Watu wenye Ulemavu Migombani Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.