Habari za Punde

Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akizungumza na Kamati ya Baraza la Mitihani Zanzibar kuhusu hatua zitazochukuliwa baada ya kufutwa Mtihani  wa Kidatu cha pili mwaka 2018 katika Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Unguja.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri akionyesha kuchukizwa na kitendo cha kuvujisha Mtihani wa Kidatu cha Pili mwaka 2018 katika mkutano na Kamati ya Baraza la Mitihani uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Unguja.
 Baadhi ya Watendaji wa Baraza la Mitihani Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma (hayupo pichani) alipokutana nao katika Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo kufuatia kuvuja  Mtihani wa Kidatu cha  Pili mwaka 2018  
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir       Maelezo      
Waziri wa Elimu mafunzo na amali Riziki Juma Pembe  alisema Wizara haitomuonea haya kwa yeyote atakaegundulika kuhusika  iwe  kuchangia au kusababisha mitihani kuvuja sheria itachukua mkondo wake hata awe mtu wa karibu.
Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa Mbadala Rahaleo wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa Baraza la mitihani kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu kuvuja kwa mitihani na kukiri kuwa mitihani mengine itafanywa hapo tarehe itapotangazwa .
Aidha alisema tumeakhirisha kwa sababu tungeendelea nayo tungefanya maamuzi siyo ya haki  kwa walokuwa hawakupata tusingeliwatendea haki.
Alisema iwapo atagundulika mtu yeyote hata awe  na ukaribu wa aina gani  gani Wizara haitoweza kumvumilia hatua za sheria za utumishi  zitachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine na tukio hili lisiweze kutokea tena.
Aliwaomba watendaji wote kuwa na ushirikiano ili ziondoke athari zilizojitokeza , pia suala la uzembe kama hili lisitokee tena watendaji wajiamini  kwani walijikubalisha na walikula kiapo hivyo waache tamaa na wawe waadilifu hata Mwenyezi Mungu anahimiza uadilifu.
“Naomba mashirikiano katika utendaji  mzima  wa kazi ili uzembe huu usitokee tena  kwani kila mtu alikula kiapo katika utendaji wake wa kazi muhali uondoke tutakwenda sambamba na nitakula nae sahani  moja ”.Alisema Waziri huyo.
Nae Naibu Waziri Mmanga  Mjengo Mjawiri  alisema  kiongozi yeyote aliyelelewa vizuri hakubali kwenda kinyume na kazi yake lazima atakuwa yuko makini na utendaji  kazi zake.
Alisema hili ni tukio la aibu limetokea na hivyo tuwe makini suala hili lisijirejee tena  kwani lineondosha uaminifu kwa jamii na hasara kwa Serikali , wanafunzi na walimu pamoja na wazee.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.