Watoto wa Skuli ya Kisiwandui wakipendezesha Kongamano kwa kuimba nyimbo ya Mwanandege wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.
Watoto wa Skuli ya Kisiwandui wakipendezesha Kongamano kwa kuimba nyimbo ya Mwanandege wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga
Sehemu ya Wadau na Wataalamu wa Kiswahili waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.
Baadhi ya Vitabu mbalimbali vilivyoonyeshwa leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Na. Mwandishi Wetu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Jamii kubadili fikra kwa kuchunguza na kufikiria jinsi ya kutumia vipengele mbalimbali vya lugha ya Kiswahili na Utamaduni wake kama bidhaa ya biashara.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama Cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).
“Sote ni mashahidi wa namna lugha ya Kiswahili imeendelea kukua kwa kasi na kuwa si lugha tena bali ni bidhaa yenye tija katika soko la utandawazi”alisema Makamu wa Rais.
Kaulimbiu ya Kongamano hilo la siku mbili inayosema KISWAHILI CHETU UMOJA WETU KWA MAENDELEO YETU limehudhuriwa na wadau na wataalamu kutoka Mataifa ya Uingereza, Poland, Marekani, Misri, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Pakistan Ujerumani na Austria.
Makamu wa Rais ameipongeza CHAKIDU kwa kuhakikisha Kiswahili hakimezwi na lugha za kigeni na kukifanya kiendelee kukita mizizi kwa kusambaa maeneo mbalimbali.
Makamu wa Rais amesema Benki ya Maendeleo Afrika ilishaonyesha njia kwa kutumia Kiswahili kwa mara ya kwanza katika chapisho lake la Uchumi hivyo basi Afrika inaweza kutumia Kiswahili na pia kikatumika kama moja ya lugha rasmi za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Kwa upande mwingine Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ametoa wito kwa Wataalam wa Lugha ya Kiswahili kuweka maazimio kwenye maeneo ambayo bado hayajafanyiwa kazi ili watu wengi zaidi wakipende Kiswahili.
No comments:
Post a Comment