Habari za Punde

Uzinduzi wa Kongamano la Pili ta Kiswahili la Kimataifa Zanzibar Lafanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Maalum Mtunzi wa Vitabu Tanzania Mzee Shafi Adam Shafi, kwa Utunzi wake wa Vitabu mbalimbali vya Kuli, Vuta N'kuvute, Haini, Kasir ya Mwinyi Fuad,na Mtoto wa Mama kilichozinduliwa leo, wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.kulia Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA Dkt. Mohammed Sheif Khatib alipowasili katika viwanja vya Idrissa Abdulwakil kuhudhulia Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume alipowasuili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Uchapaji Vitabu ya Vide Muwa. Paul Nganga, alipotembelea maonesho ya Vitabu mbalimbali wakati wa maonesho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagalia kitabu wakati akitembelea Maonesho ya Machapisho ya Vitambu vya Riwaya mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar lililofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar,kulia Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Taifa BAKIZA Dkt Mohammed Seif Khati, na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Taifa Zanzibar Dkt. Mohamed Seif Khatib, wakati alipokuwa akitembelea maonesho ya machapisho ya vitabu, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar linalofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisoma kitabu.wakati wakitembelea maonesho hayo.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Ali Mohamed Shein, akitembelea Maonesho ya Vitabu mbalimbali, wakati wa hafla ya Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa Zanzibar BAKIZA  
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Kiswahili Zanzibar BAKIZA Dkt. Mohammed Seif Khatib, akimuonesha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, chapisho la Kamusi la Kiswahili wakati alipokuwa akitembelea maonesho ya Vitabu, katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akifuatilia maelezo hayo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa Zanzibar Bi. Mwanahija Juma Ali, akitowa maelezo ya Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar, kabla ya ufunguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu wakifuatilia maelezo ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwakilishi wa Wachapishaji wa Vitabu Tanzania Ndg Gabriel Kitua,akitowa salamu kwa niaba ya Washiriki wote wanaochapisha Vitabu wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Pili la Kiswahili la Kimataifa lililozinduliwa leo katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Baadhi ya Waalikwa Wachapishaji wa Vitabu na Watunzi wakifuatilia Uzinduzi huo wa Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa linalofanyika Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Kiswahili Zanzibar BAKIZA.
Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA Dkt. Mohammed Seif Khatib, akitowa maelezo ya Kongamano hilo la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar , kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulizindua katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Abeid Karume akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar , lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdilwakil Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Pili la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.


















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.