Habari za Punde

Azam yaibuka kidedea kombe la Mapinduzi Yaifunga Simba 2-1

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Azam FC kabla ya kuanza kwa pambano la fainali kati yake na Wekundu wa msimbazi Timu ya Soka ya Simba zote za Dar es salaam.
 Nahodha wa Timu ya Soka ya Azam FC  Aggrey Morris akikabiodhiwa kikombe na Mgesni wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake chake Pemba.
Mchezaji wa Timu ya Azam FC akipokea kitita cha shilingi Milioni 15,000,000/- kama zawadi kwa kuibuka Mshindi wa Mapinduzi Cup hapo Uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba,.

Azam Sports Club ya Dar es salaam imewathibitishia Wanasoka Tanzania kwamba wao bado wanaendelea kuwa wawabe wa Mchezo huo Maarufu Duniani kwa kutetea tena Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baaada ya kuwalaza  Wekundu wa Msimbazi Timu ya Soka ya Simba pia ya Dar es salaam kwa Magoli 2 – 1.
Pambano hilo la Fainali lililoshuhudiwa na Wapenzi wa Soka kutoka Maeneo mbali mbali ya Tanzania wakifaidi zaidi wale wa Mikoa Miwili ya Kisiwa cha Pemba lilipigwa ndani ya Nyasi Bandia za Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake Chake
Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Mgeni Rasmi wa Fainali hiyo aliwaongoza wapenzi wa Soka kushuhudia mtanange huo uliowakutanisha wababe hao wa Soka Tanzania.
Azam iliyoonyesha uwezo mkubwa wa Soka tokea kuanza kwa  mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi yaliyojipatia umaarufu katika miaka ya hivi karibuni ilianza kuzitikisha nyavu za Wekundu wa Msimbazi kunako dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza lililofungwa na Mchezaji Mudathir Yahya.
Wekundu wa Msimbazi  ilipindua matokeo kusawazisha Goli mnamo dakika ya 20 Kipindi cha Pili cha Mchezo lililofungwa na Mchezaji  Yussuf  Mpilipili baada kuunganisha Mpira wa Krosi Magharibi mwa Goli la Kusini.
Mshike mshike wa pambano hilo liloshuhudiwa na maelfu ya watazamaji lilileta raha kwa kila Timu ikifanya jitihada za kujitafutia Ushindi katika mchezo huo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na mnamo dakila ya  30Mchezaji  Hadhir Chirwa wa Timu ya .Azam akaipatia goli la Pili na la Ushindi Timu yake.
Hadi Mwisho Azam FC Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi wametawadhwa tena Kombe hilo walilokabidhiwa moja kwa moja kutokana na kulichukuwa kwa Vipindi viwili mfululizo.
Wekundu wa Msimbaji waliingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitoa Malindi katika pambano lililomalizika kwa Penalti  wakati Azam wao wakatinga Failam baada ya kuwalaza Timu ya Mlandege  michezo yote hiyo ilikuwa ikifanyika Usiku katika Uwanja wa Amani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikabidhi Kikombe, Jezi, na Mipira  kwa Bingwa huyo wa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi Timu ya Soka ya Azam FC Fedha Taslim shilingi Milioni 15,000,000/- Taslin.                                                                   


Balozi Seif akamkabidhi Mshindi wa Pili Simba SC waliopata zawadi ya Kikombe, Fedha Taslim Shilingi Milioni 10,000,000/- , Jezi , Mipira pamoja na Medali kwa kila Mchezaji wa Timu hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi pia akakabidhi Kikombe Seti ya Jezi, Medani na Fedha Taslimi Shilingi Laki 750,000/- kwa Bingwa wa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwa Timu za Watoto wa Umri wa Miaka 17 ambapo Kombaini ya Wilaya ya Mjini iliibuka Mshindi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid  zawadi kwa Mshindi wa pili Kombaini ya Wilaya ya Chake iliyopata Kikombe, Seti ya Jezi, Medani kwa Wachezaji pamoja na zawadi ya Shilingi Laki 500,000/- Taslim, wakati Mshindi wa Tatu Kombaini ya Wilaya ya Wete iliyoibuka na Kikombe, Medali kwa wachezaji na Shilingi Laki 250,000/-.
Muamuzi Bora Mohamed Amour, Kipa Bora Hamad Ubwa na Mfungaji Bora Yussuf  Nassor wa mashindano hayo ya Mapinduzi Cup Watoto yaliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC} walipata zawadi ya shilingi 50,000/-  kila mmoja

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.