Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Aendelea na Ziara Yake Wilaya ya Kati Unguja leo, na Kuweka Jiwe la Msingi Skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa.

Rais swa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu alipowasili katika viwanja vya Skuli mpya ya Msingi na Maandalizi Ng'ambwa Uzi, kuweka Jiwe la Msingi leo, akiwa katika ziara yake Wilaya ya Kati Unguja.
Jengo Jipya la Skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa Uzi, lililojengwa kwa nguvu za Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa kushirikiana na Wananchi wa Kisiwa cha Uzi Unguja na kumalizia Ujenzi huo na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, na kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, wakisoma maandishi ya Jiwe la Msingi la Skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa Uzi, baada ya kuashiria kuondoa kipazia kuweka jiwe la msingi la jengo hilo, leo akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Kati Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.