Na Grace Semfuko-MAELEZO
Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa kushirikiana na
Magnet Youth Sports Organization ya Tanzania February 15 hadi 19 mwaka huu walishirikiana katika kuandaa safari ya kitalii ya kocha
andreas Pach na Martin Hammel wa
Ujerumani ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kutembelea vivutio vya Utalii lengo
likiwa ni kuutangaza Utalii wa Tanzania.
Andreas Pach na Mwenzake Martin
Hammel ni Makocha ambao wapo nchini
Tanzania wakitokea kwenye mradi wa ITK Pathfinder 2019 uliopo chini ya Chuo Kikuu
cha Leipzig cha nchini Ujerumani mradi
ambao unalenga kuwafundisha Makocha na Vijana kwenye mchezo wa Soka na kumtangaza
Mchezaji nyota mwenye asili ya Tanzania anaechezea Ligi daraja la kwanza nchini
Ujerumani Yusuph Poulsen.
Wakiwa Nchini Tanzania Makocha
hao walipata nafasi ya kutoa mafunzo ya michezo kwa makocha 25 na Vijana 120 wa
Kitanzania lengo likiwa ni kukuza Vipaji vya michezo nchini.
Ujio wa makocha hao ni mwaliko wa
Magnet Youth Sports Organization chini ya Mkurugenzi mwendeshaji wake Tuntufye
Mwambusi ambapo bodi ya utalii kupitia
ujio huo wameamua kushirikiana katika kuutangaza utalii wa ndani ikiwepo Mlima
Kilimanjaro
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema bodi hiyo imeanza mazungumzo ya wali na
mchezaji huyo nyota Yusuph Poulsen ambaye anachezea ligi daraja la kwanza
nchini Ujerumani ili kuutangaza Utalii wa ndani.
“kwetu sisi TTB tunachukulia ujio
huu wa makocha hawa na mashirikiano yaliyopo kati ya ITK na Tanzania, na
tumeanza mazungumzo na Mchezaji mwenye asili ya Tanzania Bw. Yusuph Poulsen
ikiwa ni mkakati wetu wa kutumia watu maarufu katika kuutangaza utalii wa ndani
na tunataka kumfanya kuwa Balozi wa
hiyari wa utalii wa Nchi yetu” alisema Jaji Mstaafu Thomas Mihayo.
Nae mmoja kati ya makocha hao
wawili wa kutoka Nchini Ujerumani Bw.Andreas Pach alisema Tanzania kuna Vipaji
vingi vya Michezo na hivyo ni muhimu kuviendeleza.
“tumefurahishwa kuona Watanzania
ni watu wakarimu, Tanzania kuna Vijapi vingi vya Michezo na vipaji hivi
vikiendelezwa tutakuwa mbali kimichezo, Poulsen anafanya Vizuri sana kule
Ujerumani” alisema Andreas Pach
Kwa upande wake Mkurugenzi
mwendeshaji wa Magnet Youth Sports Organization Bw. Tuntufye Mwambusi alisema
wataendelea kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na wanamichezo katika
kukuza Utalii wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment