Habari za Punde

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, Amewataka Walimu Wakuu Kisiwani Pemba Kuwasimamia Walimu Walioajiri Karibuni.


Naibu Katibu Mkuu Taaluma Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Madina Mjaka Mwinyi,akizungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari Pemba katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Madungu Chake Chake Pemba. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. MmangaMjengoMjawiri, Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Sekondari Bi AsyaIddi.


NaibuWaziriwaElimunaMafunzoyaAmali Zanzibar Mh. MmangaMjengoMjawiriakizungumzanaWalimuWakuuwaSkulizaSekondari Pemba katikaMkumbiwaSkuliyaSekondariMadunguChakeChake Pemba. KushotoniNaibukatibuMkuutaaluma Bi MadinaMjakaMwinyinakulianiAfisaMdhaminiWizarayaElimuNd. Moh’dNassorSalim.


Baadhi ya Walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Sekondari Kisiwani Pemba wakifuatilia hafla ya Mkutano na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Madungu Chakechake Pemba.

Na Suleiman Juma
Walimu Wakuu wa Skuli za sekondari kisiwani Pemba wametakiwa kuwajengea mazoea walimu wapya ili kufahamu vyema taratibu za kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri wakati akizungumza na walimu hao katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Madungu Chakechake Pemba.

Amesema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa walimu wapya ikiwemo kushindwa kufundisha kwa ufanisi hali inayochangia kufeli kwa wanaafunzi wengi Visiwani Zanzibar.

Aidha, Mhe. Mmanga amewataka walimu hao kuwapa mafunzo na mbinu za ufundishaji pamoja na taratibu za maadili ya kazi zao ndani ya mwezi mmoja baada ya kuajiriwa.

Sambamba na hilo Naibu Waziri huyo amesema Wizara ya Elimu imepanga kuanzisha utaratibu wa kukutana na walimu wazoefu kujadili juu ya mbinu mbali mbali za uboreshaji na upandishaji wa kiwango cha ufaulu.

Naye Naibu Katibu Mkuu taaluma Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi.Madina Mjaka Mwinyi amewataka walimu wakuu kutowasajili wanafunzi wanaokosa sifa za kuwa watahiniwa wanafunzi ili kupunguza kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Awali,Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Ndg.Mohammed Nassor Salim amesema hali ya utoro kwa wanafunzi imekuwa kikwazo kwa ufaulu maskulini hivyo amewataka walimu hao kutowasajili wanafunzi ambao wamekosa sifa za kufanyiwa usajili.

Akizungumzia upungufu wa walimu kwa skuli za sekondari kisiwani Pemba amesema jumla ya walimu 810 wamasomo mbali mbali wanahitajika ambao serikali ipo mbioni kutatua changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.