Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Atembelea Kambi ya JKT ya Bulombora Mkoani Kigoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja  Jenerali , Martin Busungu wakati alipowasili kwenye Kambi ya JKT ya Bulombora wilayani Uvinza, kuhamasisha ufufuaji wa zao la michikichi, Februari 17, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kushoto) wakitazama sabuni zinazotengenezwa na Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa katika Kambi ya Bulombora wilayani Uvinza wakati alipotembelea  kambi hiyo kuhamasisha ufufuaji wa zao la michikichi
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akiwasha trekta ikiwa ni ishara ya kuzindua trekta hilo katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Bulombora wilayani Uvinza, Februri 17, 2019. Mheshimiwa Majaliwa yuko mkoani Kigoma kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha ufufuaji wa zao la michikichi.
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akipanda mchikichi ikiwa ni ishara ya kuzindua upanuzi wa shamba la zao hilo katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Bulombora  wilayani Uvinza, Februari 17, 2019. Mheshimiwa Majaliwa yuko mkoani Kigoma kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha  ufufuaji wa zao la michikichi. 

 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.