Habari za Punde

. Mbunge wa Jimbo la Magomeni akabidhi Basi Jimboni


 Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Abdalla Juma Mabodi akizungumza na Wanachama  wa Chama hicho pamoja na Viongozi  kuhusu maendeleo waliyoyafanya katika Jimbo lao la Magomeni  huko Uwanja wa Mzalendo ndani ya Jimbo hilo katika Uzinduzi wa Gari aina ya Basi ya Jimbo.

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Abdalla Juma Mabodi akipokea Funguo na Kadi ya Gari aina ya Basi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim huko Uwanja wa Mzalendo katika Jimbo hilo .

 Jamal Kassim akielezea juu ya hatuwa walizofikia katika kuleta Maendeleo ya  Jimbo  huko Uwanja wa Mzalendo katika Uzinduzi wa Gari aina ya Basi ya Jimbo.
 Muwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Kigoma akielezea machache kuhusu utekelezaji  wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi huko Uwanja wa Mzalendo  Jimboni kwake katika Uzinduzi wa Gari aina ya Basi ya Jimbo hilo.
 Gari aina ya Basi iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamali Kassim hayupo pichani, yenye thamani ya Shiling Milioni ishirini na tisa na laki tano.
 Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Gari aina ya Basi ya Jimbo la Magomeni wakifatilia kwa makini shuhuli hiyo wakiwa katika Uwanja wa Mzalendo Jimboni hapo.

Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliohudhuria katika Uzinduzi wa Gari aina ya Basi ya Jimbo la Magomeni wakifatilia kwa makini shuhuli hiyo wakiwa katika Uwanja wa Mzalendo Jimboni hapo.
Picha na Maryam Kidiko.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.