Habari za Punde

Waziri Mpina Aongoza Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Utiaji Saini Udhibiti Uvuvi Haramu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mhe Luhaga Mpinaa mbaye ndiye Makamo Mwenyekit i(mwenyemiwani) wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO),inayojumuishanchiwanachamawa Afrika Mashariki akiangalia taarifa aliyotia saini ya makubaliano yakuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katikaZiwa Victoria mara baada ya kumaliza kuendesha kikao hicho jijini Arusha.Kushotoni Waziri waKilimo,WanyamanaUvuviwa Uganda, VincentBamulangakiSsempijja, kushotoniKatibuMkuuwaUvuviwa Kenya Prof. Micheni Ntiba aliyemwakilisha Waziri wake anayefuata niDkt.Deo-Guide RUREMA Waziri waMazingira ,KilimonaMifugowa Burundi. 
Watendaji,MakatibuWakuunaMawaziriwanaosimamiaSektayaUvuviwanchiWanachamawaJumuiyaya Afrika Mashariki baada ya kumaliza mkutano wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO) ambapoWaziri waMifugonaUvuviwa Tanzania MheLuhaga Mpina, ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Oganaizesheni(mwenye miwani kwa waliokaa msitari wa mbele) aliendesha kikao hicho kilicho malizika kwa kutilia na saini makubaliano ya kuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria.Pichana John Mapepele.
Mawaziri na Wawakilishi wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Uvuvi wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionyesha taarifa waliyotia saini ya makubaliano yakuendesha Operesheni ya pamoja ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria mara baada ya kumaliza kikao hicho jijini  Arusha.Mwenye miwani niMheLuhagaMpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania,Kushotoni Waziri wa Kilimo,Wanyama na Uvuvi wa Uganda, Vincent BamulangakiSsempijja,anayefuata ni Dkt. Shigalla Mahongo-KatibuMtendaji wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), kulia ni Katibu Mkuu wa Uvuvi wa Kenya Prof. Micheni Ntiba aliyemwakilisha Waziri wake na anayefuata ni Dkt.Deo-Guide RUREMA Waziri wa Mazingira ,Kilimo na Mifugo wa Burundi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania,Mhe LuhagaMpina ambaye ndiye Makamo Mwenyekiti wa Oganaizesheni ya Uvuvi wa Ziwa Victoria (LVFO), inayojumuisha nchi wanachama wa Afrika Mashariki na Mgeniwa Rasmi wa Mkutano huo akisoma hotuba yake kwenye mkutano wa(LVFO)jijini Arusha.Pichana John Mapepele

Na.John Mapepele- Arusha

Makubaliano hayo ni mkakati wa nchi hizo za Kenya, Uganda na Tanzania, kulinda rasilimali hizo ziwe endelevu na zitumike kukuza uchumi wa wananchi wa mataifahayo.  

Makubaliano hayo yamefikiwa katika Mkutano wa Mawaziri waSekta za uvuvi zinazozungukwa naZiwa Victoria, uliofanyika Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika masharikiJijini Arusha, Tanzania.

Makamu Mwenyekiti wa Mawaziri wa Sekta za uvuvi wa Jumuiyahiyo, Mhehimi wa LuhagaMpina, alisema uamuzi huo utawezesha kuongezeka kwa samaki na mazao yake katika Ziwa Victoria.

Alisema hatua hiyo itachochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi wanaozunguka ziwa hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza kipato chao.

Alisema wananchi wa Afrika mashariki wanaozungukwa na ziwa Victoria walikuwa wanalazimika kuagiza samaki kutoka nchi ambazo hazina hata maziwa,licha ya ziwa hilo kuwa na uwezo wakulisha bara la Afrika kama litatunzwa vizuri.

Alisema samaki wachanga waliokuwa ziwani chini ya sentimita 50 walikuwa asilimia 96.3lakini kutokana na jitihada zilizofanywa za kudhibiti uvuvi haramu vifaranga vimepungua hadi kufikia asilimia 62.8 kiwango ambacho kinakubalika kwa vifaranga kuwepo majini.

Pia alisema samaki wanaoruhusiwa kati ya sentimita 50 hadi 80 waliokuwa wamebaki majini walikuwa asilimia 3.3 lakini baada ya kazi ya mwaka mmoja wameongezeka hadi kufikia asilimia 32 huku wale wenye urefu wakati ya sentimita 80 hadi 85 ambao ni samaki wa ziwalifikia asilimia 0.4 lakini kwa sasa wameongezeka na kufikia asilimia 5.2 kiwango ambacho kinakubalika.

Alizipongeza Taasisi za utafiti za Kenya, Uganda na Tanzania kwa umakini na umahiri wa kukusanya taarifa za kitafiti ilikuzisaidia nchi wanachama kupanga yale ya usimamizi warasilimali za uvuvi.

“Tumefanya maamuzi makubwa ya kupanga mipango ya kufanya operesheni yapamoja ili kuwa na uwelewa wa mpango ya pamoja ya namna ya kulitunza ziwa letu na kupamba na na uvuvi haramu ya mazao ya uvuvi”alisema.

Nchi hizo zimekubaliana ziwe zimelipa madeni yote kufikia juni, mwaka huu ili kuwezeshaTaasisi ya Uvuvi ziwa victoria (LVFO) kutekeleza mipangoyake kwawakati.

AkizungumzakatikamkutanohuoKatibuMtendajiwaOganaizesheniyaUvuviwaZiwa Victoria (LVFO)Dkt. Shigalla Mahongo alisisitiza kuwa na umoja katika kuhifadhi raslimali za uvuvi katika ziwa hilo kwa kuwa idadi ya watu katika nchi wanachama wajumuiya ya Afika Mashariki kuwa ikikuwa kwa kasi na kuendelea kutegemea samaki wa ziwa hilo kwa kiasi kukubwa.

“Idadi ya watu ilikuwa milioni 23.5 mwaka 1954 wakati Sangara walipowekwa katika ziwa Victoria lakini mwaka 2018 inakadiriwa kuwa idadi ya watu iliongezeka kwa takribani mara 7 nakufikia jumla ya watu wapatao milioni 165.5 ambapo sasa inakadiriwa kufikia mwaka 2050 kuwa na zaidi ya watu milioni 323.1 hiyo inamaana kuwa itakuwa ni mara 14 ya idadi ya watu waliokuwa mwaka 1954 wakati ziwa likiwa bado nililelile” alionyaDkt. Mahongo.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.