Habari za Punde

TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA


Ndugu wananchi,
Kwanza kabisa nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Mwenye Kurehemu kwa kuendelea kuijaalia nchi yetu kuwa katika hali ya amani na utulivu mkubwa.
 Ndugu Wananchi,
Kama tunavyoelewa kwamba kila inapofika tarehe 7 Aprili ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Sheikh Abeid Amani Karume,  Jemedari Mkuu wa Mapinduzi yetu Matukufu ya tarehe 12 Januari, 1964 ambayo yaliung’oa utawala wa kisultani hapa Zanzibar. Sheikh Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi katika eneo la ukumbi wa iliyokuwa Afisi Kuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui tarehe 7 Aprili mwaka 1972. Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume yana lengo la kumkumbuka kiongozi wetu huyu pamoja na viongozi wetu wengine wote waasisi wa Taifa letu waliotangulia mbele ya haki.
 Ndugu Wananchi,
Kutokana na azma hiyo, Serikali imeamua kuanzia mwaka huu wa 2019, maadhimisho haya yatafanywa kwa wiki moja kuanzia tarehe 2 Aprili na kufikia kilele chake tarehe 7 Aprili. Maadhimisho haya yatahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya ziara na kusomwa dua katika makaburi ya viongozi wakuu wa kitaifa waliokwishafariki dunia pamoja na kufanya makongamano yenye mnasaba na historia na mchango wa Mzee Karume katika maendeleo ya Zanzibar. Shughuli hizi zitafanyika Unguja na Pemba.
Ndugu wananchi,
Kufuatia utaratibu huu mpya wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Karume, kwa mwaka huu wa 2019 ratiba ya maadhimisho hayo itakuwa kama ifuatavyo:-
Siku /Muda
Tukio
Sehemu
J’nne, 2 April 2019
Saa 3.00 Asubuhi
Kufanya Ziara na kusoma dua kwenye kaburi la Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi
Migombani, Wilaya ya Mjini
Kufanya Ziara na kusoma dua katika Kaburi la Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Marehemu Dkt. Omar Ali Juma
Wawi, Wilaya ya Chakechake
Kufanya ziara na kusoma dua katika Kaburi la Marehemu Sheikh Thabit Kombo
Chukwani Wilaya ya Magharibi B
J’tano, 3 April 2019; Saa 3.00 Asubuhi
Kufanya ziara na kusoma dua katika Kaburi la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Nne Marehemu Sheikh Idris Abdul Wakil

Makunduchi, Wilaya ya Kusini 
Ijumaa 5 April 2019 Saa 3.00 Asubuhi
Kongamano la Kumuenzi Sheikh Abeid Amani Karume – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Kwanza

Ukumbi wa Makonyo, a Chake chake Pemba
J’mosi 6 April 2019 Saa 3.00 Asubuhi
Kongamano la Kumuenzi Sheikh Abeid Amani Karume – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Kwanza
Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni, Unguja
Mapokezi ya Maandamano ya Vijana ya Siku ya Karume
Kisiwandui, Wilaya ya Mjini Unguja
J’pili 7 Aprili 2019 Saa 1.00 Asubuhi
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Karume
Kisiwandui , Wilaya ya Mjini Unguja

Ndugu wananchi,
Kwa mnasaba huo, Napenda kuchukua fursa hii kuwaalika rasmi ku
hudhuria katika matukio hayo kwa siku, muda na sehemu zilizoainishwa. Ili kuhakikisha shughuli hii inafanyika kwa amani na utulivu mkubwa, siku ya Jumapili ya tarehe 7 Aprili, 2019 kuanzia saa 12:00 Asubuhi mpaka saa 7:00 Mchana, barabara ya Michenzani ‘round about’ hadi  Mkunazini itafungwa kwa vyombo vyote vya usafiri.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Zanzibar
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.